Hizi Hapa Ndio Sifa na Bei za Google Pixel 3 na Pixel 3 XL

Zifahamu kwa undani hizi ndio sifa kamili na bei ya Simu mpya za Pixel 3
Sifa na bei za Google Pixel 3 na Pixel 3 XL Sifa na bei za Google Pixel 3 na Pixel 3 XL

Kampuni ya Google hapo jana ilizindua simu zake mpya za Google Pixel 3 pamoja na Google Pixel 3 XL, kama jinsi tetesi zilivyo kuwa simu hizi hazina tofauti sana na simu za Google Pixel za mwaka jana bali kwa mwaka huu simu hizo zinakuja na kioo kikubwa pamoja na battery kubwa.

Japokuwa tetesi zilikuwa sahihi lakini bado yapo mambo mengi ambayo tungependa kukujulisha kuhusu sifa pamoja na bei ya simu hizi mpya kutoka kampuni ya Google, na bila kupoteza muda twende tukangalie yaliyomo kwenye simu hizi.

Tukianza na kioo, simu hizi za Google Pixel 3 zinakuja na vioo vikubwa tofauti na simu za Pixel 2 za mwaka 2017, Pixel 3 yenyewe inakuja na kioo cha Inch 5.5 ambacho ni sawa na kioo cha Pixel 2 lakini kioo hicho kimeongezeka kwa uwiano na sasa uwiano wa kioo hicho ni 18:9 ambayo hii ina ipa simu hii ongezeko la asilimia 10 ukilinganisha na simu ya Pixel 2 ya mwaka jana. Pixel 3 XL yenyewe inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.3 ambacho kinakuja na uwiano wa 18.5:9.

Advertisement

Tukiangalia upande mwingine wa battery, Simu ya Google Pixel 3 XL inakuja na battery yenye ukubwa wa 3,430mAh battery huku simu ya Google Pixel 3 yenyewe ikiwa inakuja na battery yenye ukubwa wa 2,915mAh ambayo hii imeongezeka ukilinganisha na simu ya mwaka jana ya Pixel 2. Simu zote zinakuja na teknolojia ya Fast Charging na zinaweza kuchajiwa kwa kutumia chaji ya wireless ambayo inaweza kuchaji simu hizo na kudumu na chaji kwa masaa 7 baada ya kuchaji simu hiyo kwa dakika 15 pekee.

Tukiangalia kwenye upande wa kamera, Simu hizi za Google Pixel 3 na Pixel 3 XL zote zinakuja na kamera moja kwa nyuma yenye uwezo wa Megapixel 12.2 ambayo ina optically stabilized image sensor (yenye 1.4µm pixels) pamoja na lens yenye focal f/1.8. Ubora wa kamera hii uko zaidi kwenye mfumo kwani Google wameongeza vitu vingi sana kwenye kamera hii. Moja ya sehemu ambazo zimeongezwa kwenye mfumo wa kamera hizo ni pamoja na Top Shot, sehemu hii itakuruhusu kuweza kupiga picha kwa usahihi hata kama ulipiga picha kwa kukosea kwa kukupa marekebisho ya picha hata baada ya kupiga picha yenyewe.

Kwa mbele simu hizi zinakuja na kamera mbili ambazo zote zinakuja na uwezo wa Megapixel 8 lakini zinatofautiana lensi kwani lensi moja inakuja na lensi yenye kuchukua wide-angle nyuzi 97 na nyingine inakuja na lensi ya kawaida yenye kuchukua nyuzi 75. Sifa nyingine za Pixel 3 na Pixel 3 XL ni kama zifuatazo.

Sifa za Google Pixel 3

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 5.5 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2160 pixels, na uwiano wa 18:9 ratio (~443 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.5 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.6 GHz Kryo 385 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele huku zote zikiwa na uwezo wa Megapixel 8 moja ikiwa na f/1.8, 28mm (wide), PDAF na nyingine Megapixel 8 ikiwa na f/2.2, 19mm (ultrawide), no AF.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, OIS, dual pixel PDAF. Huku ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 2915 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa tatu za Clearly White, Just Black na Not Pink.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM lakini pia unaweza kutumia eSim (laini ya simu inayo unganishwa koja kwa moja na kampuni ya simu na sio ile ya kadi), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi IP68 (inakaa kwa dakika 30 kwenye maji yenye urefu wa mita 1.5).
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Kwa upande wa sifa za Pixel 3 XL hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya kuwa simu hii ya Google Pixel 3 inakuja na kioo kikubwa na pia inakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch pia inakuja na battery kubwa zaidi kuliko Pixel 3.

Sifa za Google Pixel 3 XL

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.3 chenye teknolojia ya P-OLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1440 x 2960 pixels, na uwiano wa 18.5:9 ratio (~523 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.5 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.6 GHz Kryo 385 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM845 Snapdragon 845 (10 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 630.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili simu moja inakuja na GB 64 na nyingine inakuja na GB 128 zote zikiwa Hazina uwezo wa kuongezewa na memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM GB 4.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili kwa mbele huku zote zikiwa na uwezo wa Megapixel 8 moja ikiwa na f/1.8, 28mm (wide), PDAF na nyingine Megapixel 8 ikiwa na f/2.2, 19mm (ultrawide), no AF.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Megapixel 12 yenye f/1.8, 28mm (wide), 1/2.55″, 1.4µm, OIS, dual pixel PDAF. Huku ikiwa inasaidiwa na Auto HDR, Panorama pamoja na flash ya Dual-LED flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 3430 mAh battery yenye teknolojia ya Fast battery charging 9V/2A 18W
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 3.1 Type-C 1.0 reversible connector.
 • Rangi – Inakuja kwa tatu za Clearly White, Just Black na Not Pink.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Moja ya Nano-SIM lakini pia unaweza kutumia eSim (laini ya simu inayo unganishwa koja kwa moja na kampuni ya simu na sio ile ya kadi), Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack. Inakuja na teknolojia ya kuzuia maji na vumbi IP68 (inakaa kwa dakika 30 kwenye maji yenye urefu wa mita 1.5).
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, compass na barometer.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa nyuma).

Bei ya Google Pixel 3 na Pixel 3 XL

Kwa upande wa bei ya simu hizi za Google Pixel 3, simu hizi zitaanza kupatikana nchini marekani kuanzia tarehe 19 mwezi huu wa kumi na kuanzia tarehe 2 mwezi wa kumi na moja simu itapatikana huko nchini Europe. Bei zake zitakuwa zina anzia dollar $800 kwa Pixel 3 ambayo ni sawa na Tsh 1,831,000 bila kodi na dollar $900 kwa Pixel 3 XL ambayo ni sawa na Tsh 2,059,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use