Yote Yanayotarajiwa Kwenye Uzinduzi wa Simu za Google Pixel 3

Na huu ndio Muonekano wa simu mpya za Google Pixel 3
Muonekano wa simu mpya za Google Pixel 3 Muonekano wa simu mpya za Google Pixel 3

Kampuni ya Google hivi leo inafanya tamasha rasmi la uzinduzi wa simu zake mpya za Google Pixel 3, Kama ilivyo kwenye toleo la mwaka uliopita simu hizo mpya za Google Pixel zinajikita zaidi kwenye ubora wa kamera pamoja na utumiaji wa mfumo wa AI pamoja na mfumo wa Google Assistance.

Hata hivyo japo kuwa leo nduo uzinduzi wa simu hizo lakini kwa mwaka huu kampuni ya Google imefanya uzembe mkubwa kwa kushindwa kuzuia kikamilifu muonekano wa simu hiyo kuvuja kwani simu hizi za Google Pixel 3 pengine ndio simu zilizovuja zaidi kuliko simu yoyote ambayo imewahi kuzinduliwa mwaka huu 2018. Muonekano wa simu hizi ulianza kuvuja mapema mwezi wa sita mwaka huu 2018 huku picha mbalimbali zikionyesha muonekano wa simu hizo kutoka juu mpaka chini.

Pengine unaweza kujiuliza ni kwanini hapa Tanzania Tech hatukuweza kuandika sana kuhusu tetesi hizo ambazo zilikuwa zinasambaa sana kwa kipindi chote hiki, majibu ya swali hilo ni kuwa simu za Google pixel ni moja kati ya simu ambazo kweli hazijafika sana hapa Tanzania au Afrika Mashariki kwa ujumla, simu hizi zimekuwa zikitumiwa sana na watu wa bara la ulaya na kwa hapa Tanzania binafsi yangu sijapata nafasi bado ya kuweza hata kuiona live simu yenyewe.

Advertisement

Lakini maneno yangu sio sheria inawezekana simu hizi ziko hapa nchini Tanzania na kama wewe ni mmoja wa watu ambao unafahamu mahali kwenye duka linalo uza simu za Google Pixel hapa Tanzania basi wasiliana nasi kupitia fomu ya maoni hapo chini… anyway tukiachana na hayo labda twende tukangalie yale yote yanayo tarajiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa simu hizi mpya za Google Pixel 3.

  • Simu Mpya za Google Pixel 3

Tukianza na simu zenyewe hivi leo kampuni hiyo inatarajia kuzindua simu za Google Pixel ambazo kwa muonekano hazijabadilika sana kwa muonekano ukilinganisha na simu za Google Pixel 2 za mwaka jana, bali tofauti iliyopo kwenye simu za Google Pixel 3 mwaka huu zinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch. Sasa kwa mujibu wa mvujishaji maarufu Evan Blass hapo chini huo ndio muonekano wa simu hizo mpya za Google Pixel 3.

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hiyo aliyotuma mvujishaji huyo kwenye mtandao wa Twitter, Simu hizo zinakuja na muonekano sawa na Google Pixel 2 isipokuwa simu hizi ni kubwa kidogo na pia zinakuja na ukingo wa juu maarufu kama notch, mbali na hayo hizi hapa ndio sifa za Google Pixel 3.

Simu hizi zitakuwa zinatumia processor za Snapdragon 845, GPU ya Adreno 630 RAM ya GB 4 au Zaidi pamoja na Ukubwa wa ndani wa GB 64 au GB 128 huku simu nzima ikitegemewa kuendeshwa na mfumo mpya wa Android 9 Pie. Japo kuwa simu hii inaonekana kuvuja sana, lakini inawezekana kabisa Google kuna kitu ambacho wameandaa ambacho kitawashangaza wapenzi wa kampuni ya Google na simu za Google pixel kwa ujumla, hivyo basi kama wewe ni mmoja wa watu wanaotaka kujua zaidi kuhusu simu hii mpya ya Google hakikisha hupitwi kwani tutakuwa mubashara kabisa tukikuletea matangazo ya uzinduzi wa simu hii moja kwa moja kupitia hapa Tanzania Tech.

  • Tablet Mpya ya Pixel Slate tablet

Bidhaa nyingine ambayo inatarajiwa kuzinduliwa kwenye mkutano huu wa leo ni pamoja na Tablet mpya ya Pixel Slate. Kwa mujibu wa tetesi kutoka kwa Evan Blass tablet hiyo itakuja na keyboard ya kuunganisha kama ilivyo kwenye kompyuta nyingi za 2 in 1.

Tablet hii kama ilivyo simu za Google Pixel yenyewe pia inatarajiwa kuja na mfumo mpya wa Android 9 pamoja na sehemu za Google Assistant pamoja na AI moja kwa moja kwenye tablet hiyo. Mbali na hayo mambo mengine ya ziada yanayotarajiwa kwenye uzinduzi huo ni pamoja na kutangazwa kwa maboresho ya earphone za Pixel Buds, maboresho ya Google Home pamoja na maboresho mengine mengi ya programu mbalimbali za Google.

Kama umefanikiwa kusoma makala hii hadi hapa basi na uhakikisa sasa utakuwa unajua yote yanayo tarajiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa simu za Google Pixel 3 unaotegemewa kufanyika leo tareha 9 mwezi wa 10 hapo saa 11 kwa saa za Afrika mashariki. Hakikisha upitwi na uzinduzi huo kwani tutakuwa mubashara tukionyesha matangazo hayo moja kwa moja.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use