Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Kama unataka kuanza kurekodi video za YouTube hizi ndio programu bora
Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure) Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye channel ya YouTube na ungependa kufanya video zako zionekane za kisasa na za kuvutia basi ni vyema kufahamu list hii ya programu bora za bure za kuedit video kwenye kompyuta.

Kumbuka programu zilizopo kwenye list hii nyingi ni za bure kwa asilimia 100 na pia zipo baadhi ya programu ambazo zinapatikana bure lakini pia unaweza kulipia ili kuwa na uwezo wa kuzitumia zaidi, lakini pamoja na hayo programu hizo zimeingia kwenye list hii kutokana na uwezo wake wa kufanyakazi vizuri hata kwenye toleo la bure bila kulipia hata Tsh 10.

Advertisement

Najua umechoka na unapenda kujua programu hizi haraka iwezekanavyo, sasa basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende tukangalie list hii. Kumbuka programu hizi zinafanya kazi kwenye mifumo yote ya kompyuta yaani Windows, Mac pamoja na Linux.

Lightworks

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Lightworks ni programu nzuri sana kwa kuedit video, programu hii imetumika kuedit movie kadhaa za hollywood kama vile The Wolf of Wall Street, Heat, Hugo, Road to Perdition na filamu nyingine nyingi. Programu hii ni nzuri sana na inakuja ikiwa na toleo la kulipia, kitu kizuri ni kuwa toleo la bure lina kila kitu ambacho utakuwa unataka pale utakapo kuwa unataka kuanza kuedit video zako, unaweza kusoma jinsi ya kutumia programu hii kwenye tovuti ya programu hiyo.

Download Hapa

OpenShot

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

OpenShot ni programu nyingine ya bure ambayo unaweza kutumia kuedit video, programu hii inakaribia kila kitu ambacho unahitaji kuedit video. Openshot inakuja na uwezo mkubwa sana hadi wa kutengeneza video za 4K, mbali na hayo programu hii ni rahisi kutumia pengine kuliko programu nyingine kwenye list hii hivyo kama ndio unafikiria kuanza kuedit video basi hii ndio programu bora kwako. Openshot ni programu ya bure kabisa na haina haja ya kulipia.

Download Hapa

Shotcut

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Opencut ni kama programu iliyotoka ya Openshot, programu hii nayo inakuja na uwezo mkubwa wa kuedit video huku ikiwa na uwezo wa kutengeneza video hadi za 4K. Tofauti iliyopo kati ya Openshot na Shotcut ni kuwa programu hii inaugumu flani wa kutumia lakini ukisha jua jinsi ya kuitumia basi na kuhakikishia utaipenda programu hii. Programu hii ni ya bure kwa asilimia 100 hivyo usiwe na wasiwasi wa kuweza kulipia kwa namna yoyote.

Download Hapa

Hitfilm Express

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Kama wewe unataka kuedit video zako kwa utaalam zaidi basi jaribu programu hii ya Hitfilm Express, programu hii inakuja na mkubwa sana uwezo wa kuedit video na inakuja na templents pamoja na effects zaidi ya 400. Programu hii ni ya bure lakini ukitaka uwezo zaidi inabidi kununua addon ambazo zinapatikana kwenye tovuti ya programu hii kuanzia dollar $10 ambayo ni sawa na takribani Tsh 24,000.

Download Hapa

Davinci Resolve

Programu Bora za Kuedit Video Kwenye Kompyuta (Bure)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wako makini na wanataka kufanikiwa hasa kwenye swala la kuedit video basi Davinci Resolve ni moja ya programu bora sana ya kuedit video. Programu hii ni rahisi sana kutumia na inayo mambo mengi sana na ukweli kabisa ukianza kutumia programu hii utaacha kabisa kuitumia. Davinci Resolve inakuja na uwezo wa kutengeneza video za 4K, uwezo wa kurekebisha rangi pamoja na aina mbalimbali za Effects pamoja na Transitions. Ukweli mpaka sasa sijaona programu ya bure ya kuedit video bora kama Davinci Resolve.

Download Hapa

Na hizo ndio programu bora za bure ambazo unaweza kuzitumia kuedit video kwenye kompyuta, kumbuka unaweza kutumia programu hizi kwenye kompyuta yako ya Mac, Windows au Linux. Kama unataka programu nzuri za kuedit video kwenye simu unaweza kusoma hapa.

5 comments
  1. Nawezaje Kupata hii elimu kwa ukamilifu mfano Kuflash Simu,unlock, kutoa Frp,password, pn na kuweka imei.asanten

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use