App Kutoka Google Itakayo Kufundisha Web na App Design

Utaweza kujifunza CSS, HTML pamoja na Java Script yote kupitia simu yako
App ya Grasshopper App ya Grasshopper

Kama umekua ukitamani kujifunza kutengeneza website au programu mbalimbali basi hii ni yako. Wafanyakazi wanao tengeneza programu za majaribio kutoka kampuni ya Google (Area 120) wamejiunga pamoja na kuleta App ambayo itakusaidia wewe kuweza kujifunza ku-code au kutengeneza programu au App mbalimbali.

App hiyo Mpya, itaweza kukusaidia wewe kujifunza lugha mbalimbali za kompyuta kama vile HTML, CSS lakini zaidi itakufundisha lugha ya JavaScript, huku ikikupa uwezo wa kufanya majaribio madogo madogo ambapo utakuwa ukizawadiwa point kila unapo faulu majaribio hayo.

Kiukweli App hii ni nzuri sana kwa mtu yoyote ambaye anapenda kujifunza ku-programu au ku-code, kwani app hii ina njia muhimu na nzuri kuweza kumuelekeza mtu yoyote ambaye hajui kabisa kutengeneza ku-programu. Japokua mimi nina kaujuzi kidogo cha programu lakini kiukweli nimeipenda sana app hii kwani ni bora kupotezea nayo muda uku unajifunza, kuliko kutembelea mitandao ya kijamii bila faida yoyote.

Advertisement

Kwa sasa unaweza kuipata App hii kwa kuipakua kwenye soko la Play Store pamoja na App Store au unaweza kubofya hapo chini ili uweze kupakua programu hiyo inayo endana na mfumo wa simu yako.

Download App Hapa

Download App Hapa iOS

Kama utafanikiwa kuweza kuitumia App hii tuambie maoni yako unaonaje app hiyo..? Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua website ambazo zitakufundisha kucode bure. Kwa maujanja zaidi tembelea Tanzania Tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use