Zuia Watu Usio Wajua Kukuunga Kwenye Group WhatsApp

Sasa utaweza kuchagua ni nani atakualika kwenye Group la WhatsApp
Zuia Watu Usio Wajua Kukuunga Kwenye Group WhatsApp Zuia Watu Usio Wajua Kukuunga Kwenye Group WhatsApp

Ni wazi kuwa kila mtu ameshakutana na usumbufu kama huu wa kuwekwa kwenye Group la WhatsApp bila hata kumjua mtu aliye kuweka kwenye Group hilo, hii imekuwa ni kero kwa muda mrefu sana na hatimaye sasa imepatiwa ufumbuzi.

Kama unakumbuka mwezi mwaka 2019, WhatsApp ilitangaza kuwa ipo mbioni kuleta sehemu mpya ambayo itasaidia sana kuzuia watu kukualika kwenye magroup bila ruhusa yako, sehemu hiyo sasa inapatikana kwenye programu ya WhatsApp.

Zuia Watu Usio Wajua Kukuunga Kwenye Group WhatsApp

Advertisement

Kwa mujibu wa WhatsApp, ili kupata sehemu hiyo unatakiwa kuingia kwenye programu yako ya WhatsApp kisha bofya sehemu ya Settings > Account > Privacy > kisha chagua menu mpya iliyoandikwa Groups. Hapo utaweza kuona Menu mpya yenye Maelezo yenye kutaka uchague ni nani atakaye weza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp.

Kila sehemu inayo maana yeka na ni muhimu kuzingatia ni menu unayochangua ili kuweza kuzuia watu sahihi kukualika kwenye magroup.

  • Everyone – Pale utakapo changua sehemu hii utaweza kuruhusu watu wote kukualika kwenye magroup ya WhatsApp na hii ndio Menu inayokuwepo mara unapo ingia kwenye ukurasa huu.
  • My Contacts – Pale utakapo chagua menu hii utaweza kuruhusu watu wote ulio save namba zao kwenye simu yako kuweza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp.
  • My contacts Except – Hapa utaweza kuchagua ni watu gani au mtu gani mmoja au zaidi wataweza kukualika kwenye magroup ya WhatsApp, hapa unaweza kuzuia watu wote kwa kuchagua alama ya tiki iliyopo juu upande wa kulia ndani ya majina yatakayo funguka baada ya kuchagua sehemu hiyo.

Hata hivyo watu wote ambao watakua hawana uwezo wa kukualika kwenye magroup wataruhusiwa kukutumia meseji binafsi, meseji ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu hadi siku tatu na baadae kuacha kufanya kazi.

Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwa watumiaji wa programu ya WhatsApp ya Android na iOS na unaweza kupata sehemu hii kama unatumia toleo jipya la programu ya WhatsApp. Mbali na hayo WhatsApp pia imeweka sehemu ya ulinzi wa fingerprint kwenye programu yake ya Android na unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuwasha sehemu hiyo.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use