Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Utaweza kuficha likes au views kwenye post moja au kwenye post zako zote
Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Instagram ni moja kati ya mtandao ambao unatumiwa na watu wengi zaidi hasa hapa Tanzania, kutokana na umuhimu wa mtandao huu, idadi ya likes kwenye picha imekuwa ni kitu cha muhimu sana kwa watu mbalimbali.

Mbali na hayo, likes pia zimekuwa kama sehemu ya kuonyesha umaarufu wa akaunti kwa watumiaji wengine na hivyo kufanya watumiaji kuangalia likes zaidi na sio kutengeneza post nzuri zenye kuvutia watu zaidi.

Advertisement

Kuliona hili, Instagram imekuja na njia ambayo itafanya watu wasijue idadi ya likes au views unazopata kwenye picha au video yako na hivyo kufanya kuweka usawa kwa watumiaji wengi.

Kupitia makala hii nitakuonyesha njia hiyo ambayo inaweza kukusaidia kuficha idadi ya likes na views kwenye akaunti yako ya Instagram kwa urahisi sana.

Ficha Idadi ya Likes na Views Instagram

Kwa kuanza hakikisha una update app ya Instagram kupitia soko la Play Store au App Store, baada ya ku-update moja kwa moja fuata hatua hapo chini.

Bofya vitufe vitatu vilivyopo juu upande wa kushoto, baada ya hapo bofya sehemu ya settings iliyopo chini kabisa baada ya kubofya vitufe vitatu.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Baada ya hapo bofya sehemu ya Privacy, kisha chagua sehemu ya Posts. Sehemu hii inakuwepo kama ume update app yako ya Instagram. Kama huja update app yako unaweza usione sehemu hii, pia kumbuka kuna wakati unaweza usione pia sehemu hii lakini kuna njia unaweza kutumia.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Baada ya hapo, utaweza kuona sehemu mpya ya Hide Likes and Views Counts, bofya kuwasha sehemu hii.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Baada ya kuwasha sehemu hii, funga na fungua akaunt yako ya Instagram na moja kwa moja hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kuona idadi ya likes kwenye picha na views kwenyevideo zako isipokuwa wewe mwenyewe.

Kumbuka pia hata wewe hutoweza kuona idadi ya likes na views kwenye picha za watu mbalimbali ambao umewafuata (Follow) kupitia akaunti yako. Utakapo zima sehemu hii basi moja kwa moja utaweza kuanza kuona idadi ya likes na views za watu wengine, na watu wengine pia wataweza kuona idadi ya likes na views kwenye picha na video zako.

Ficha Likes na Views Kwenya Post Moja (Kwa Post Mpya)

Kama unataka kuficha likes na views kwenye picha au video moja mpya ambayo unapost basi unaweza kufuata hatua hapo chini.

Kwa kuanza bofya kitufe cha kupost picha yako au video, kisha baada ya kuandika maelezo au caption bofya kitufe cha Advanced Settings, mwisho kabisa wa kurasa.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambapo unatakiwa kubofya na kuwasha sehemu iliyo andikwa Hide Like and View Counts on This Post.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Baada ya hapo, rudi mpaka kwenye ukurasa wa kupost na unaweza kupost moja kwa moja na post hiyo haita onyesha idadi ya likes au views kwa wafuasi wako.

Ficha Likes na Views Kwenye Post Moja (Post za Zamani)

Kama unataka kuficha idadi ya likes na views kwenye post moja ambazo ni post za zamani au ambazo umesha post muda mrefu unaweza kufanya hivyo kwa kufuata hatua hapo chini.

Fungua au nenda kwenye post ya Instagram ambayo unataka kuficha idadi ya likes au views, baada ya hapo bofya vitufe vitatu kwenye post husika, Baada ya hapo ukurasa mpya utafunguka kisha angalia mwisho wa ukurasa huo na utaweza kuona sehemu ya Hide Like Count bofya hapo kuficha idadi ya likes au views.

Jinsi ya Kuficha Likes na Views Akaunti Yako ya Instagram

Kwa kufanya hatua hizo utaweza kuficha idadi ya likes au views kwenye post zako za Instagram, kumbuka kwa kuficha lkes na views kwenye picha moja moja utaendelea kuona likes kwenye picha nyingine za wafuasi wako na hata kwenye picha zako.

Lakini kwa kutumia njia ya kwanza kwenye makala hii wewe binafsi huweza kuona views na likes kwenye post nyingine za akaunti ulizo zifuata kwneye mtandao wa Instagram. Kama unataka kuendelea kuona views na likes za watu wengine ni bora kutumia njia ya kwanza na ya pili.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use