Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mabadiliko Makubwa kwa Ma-Admin wa Magroup ya WhatsApp

Sasa admin ataweza kumondoa admin mwenzake bila yeye kujua
whatsapp admin group whatsapp admin group

Kwa sasa ni wazi kuwa ni watu wengi sana wanatumia magroup ya WhatsApp kuwasiliana, lakini pia pamoja na umuhimu wa magroup haya lakini baadhi ya ma-admin wa magroup haya wamekuwa hawana ustaarabu, kuona hilo sasa WhatsApp imeleta mabadiliko kwa upande wa ma-admin.

Hivi karibuni WhatsApp imeanza kujaribu sehemu mpya ambayo sasa admin ataweza kumuondoa admin mwingine kwenye group bila kumtoa kabisa kwenye group. Yaani hapa ina maana kuwa, kama group lina admin zaidi ya mmoja basi admin mmoja anaweza kumvua u-admin mwenzake na kumfanya kuwa mshiriki wa kawaida wa group bila kumuondoa kabisa kwenye group.

Advertisement

Hapo hawali ilikuwa, kama wewe ni admin na unataka kumvua u-admin admin mwingine basi ni lazima muondoe kabisa kwenye group kisha ndio umrudishe kama mchangiaji wa kawaida lakini sasa utaweza kumvua u-admin admin mwenzako bila hata yeye kujua.

Kwa sasa sehemu hii iko kwenye hatua za majaribio kupitia programu ya WhatsApp Beta ya Android na pengine siku sio nyingi ma-admin wote wataweza kuona sehemu hiyo mpya.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use