Hivi karibuni mtandao wa Instagram unategemewa kuongezewa maboresho mengine kwenye sehemu maarufu ya Stories, maboresho hayo yana husisha aina mpya ya stories ambayo imepewa jina la Type.
Aina hii sio mpya sana kwani ni kama ile iliyopo kwenye programu ya WhatsApp ambapo unaruhusiwa kuweka Status ya maandishi yenye rangi badala ya picha.
Sehemu hii inategemea kuja kupitia sehemu ya Stories na inapatikana kuptia option ambayo ita andikwa Type, pembeni ya sehemu zile za kwenye stories za Boomerang pamoja na Rewind.
Mbali na hayo kwa mujibu wa tovuti ya Wabetainfo, Instagram inategemea kuleta sehemu nyingine kupitia sehemu hiyo hiyo ya Stories ambapo sasa utapewa taarifa pale mtu atakapo chukua screen-shot ya picha, video au maandishi utakayokuwa umeweka kupitia sehemu ya Stories.
Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo, pale utakapo chukua screenshot kwa mara ya kwanza utaweza kupewa onyo na kama ikitokea umerudia kuchukua screenshot kwenye sehemu ya Stories basi, mwenye Stories hiyo atatumiwa ujumbe kuwa umechukua screenshot.
Sehemu hizi zinategemewa kuja kwenye programu za Android na iOS siku za karibuni, kwa sasa bado hakuna taarifa kamili juu ya sehemu hii itatoka lini kwa taarifa kamili endelea kutembelea ukurasa huu tutakupa taarifa tutakapo pata taarifa kamili.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.
alimtamu msanii muigizaji na mui,mbaji natafuta uzamini 0745529428
nawapenda sana amani