Sasa Angalia Video za YouTube Ndani ya App ya WhatsApp

Sasa utaweza kuangalia video za youtube kupitia app ya Whatsapp
WhatsApp iOS WhatsApp iOS

Hivi karibuni kupitia App ya majaribio ya WhatsApp Beta, ilikugundulia njia mpya ambayo ilikuwa kwenye majaribio njia ambayo ilikuwa ikiwezesha mtu kuangalia video za YouTube ndani ya App ya WhatsApp.

Hivi karibuni sehemu hiyo imekuja rasmi kwenye App ya WhatsApp ya mfumo wa iOS, na sasa watumiaji wa app hiyo wataweza kuangalia video za youtube ndani ya app WhatsApp.

Advertisement

Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwenye wenye simu za iOS pekee na inawezeshwa kwa kutuma link kwa mtu na mpokeaji moja kwa moja ataweza kuangalia video ndani ya App ya WhatsApp bila kuingia kwenye app ya YouTube. Kwa watumiaji wa simu za Android itabidi kusubiri kidogo kwani sehemu hii inatarajiwa kuja kwenye simu hizo hivi karibuni, ili kujua lini sehemu hii itakuja kwenye simu yako kaa karibu nasi na endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

3 comments
  1. Mushi,
    Nimeangalia kwenye simu yangu ya iPhone hiyo option ya kuangalia link ya Youtube moja kwa moja kupitia Whatsapp app haipo na sijaona bado Update ya Whatsapp yenye maboresho hayo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use