Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Programu Mpya za Kuedit Picha Mwaka Huu 2018

Jaribu programu hizi mpya ambazo zitakusaidia kuedit picha mwaka 2018
programu za kuedit picha 2018 programu za kuedit picha 2018

Ni kweli kuwa wengi wetu tunapenda picha na kwa namna moja ama nyingine picha ni sababu ya watu wengi kuwa na aina flani ya smartphone, lakini smartphone bila kuwa na programu bora za kufanya picha ionekane tofauti ni sawa na kuwa na gari bila magurudumu.

Kusaidia kwenye hilo leo Tanzania Tech tunakuletea App mpya kabisa za mwaka 2018, ambazo zitasaidia picha zako kuwa na muonekano wa tofauti na wa kisasa kabisa. Kumbuka app hizi zinapatikana bure kabisa na zote zinapatikana kupitia masoko ya Android na iOS. Bila kupoteza muda twende tukaziangalie app hizi.

Advertisement

  • Lens Distortions Android
Photo Effects - LD
Price: Free
  • Lens Distortions iOS

Lens Distortions hii ni App mpya kabisa itakayo kusaidia ku-edit picha zako kwa namna ya tofauti kabisa, app hii itakupa uwezo wa kuweka effect mbalimbali kwenye picha zako, vilevile kupitia app hii utaweza utaweka kuweza filter za tofauti na mpya kabisa. Jaribu sasa App hii kwa kuidownload kwa kubofya hapo juu.

  • AfterFocus Android
AfterFocus
Price: Free
  • AfterFocus iOS
‎AfterFocus
Price: $0.99

AfterFocus ni app nyingine mpya ya kuedit picha kwa mwaka 2018, App hii itakupa uwezo wa kuedit picha na kuongezea uwezo wa kugarisha sehemu flani ya picha na kuongezea mwanga picha yako pamoja na kufanya kuonekana zaidi, app hii ina uwezo mkubwa sana na itakupa njia mpya za kuedit picha yako kwa mwaka 2018.

  • Vimage Android
  • VimageiOS

Vimage ni app nyingine mpya ambayo hii itakupa uwezo wa tofauti sana, app hii itakusaidia kutengeneza picha zinazo tembea kwa kuweka effect mbalimbali kama mwanga, moshi na effect nyingine nyingi zinazo tembea ndio maana ya kuitwa vimage ikiwa na maana ya Video Image, jaribu sasa app hii na uhakika utaifurahia.

Tofauti na programu zingine programu hizi zitakupa njia mpya kabisa za kuedit picha na zita kusaidia kupata picha za tofauti zenye effect na filter mpya kabisa za mwaka 2018. Pia unaweza kusoma list ya app bora za kuedit picha kwa mwaka 2017 ili kupata style ya picha inayofaa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use