Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

LG Yazindua LG K7i Simu Yenye Uwezo wa Kufukuza Mbu

Sasa simu yako inauwezo wa kukusaidia kupambana na Mbu
LG K7i LG K7i

Wakati teknolojia ikiendelea kukua kwa kasi ya aina yake kampuni kubwa ya vifaa vya umeme ya LG hivi karibuni imezindua simu yake mpya ya LG K7i, lakini simu hii sio kama simu nyingine bali simu hii imewezeshwa na teknolojia ya kufukuza na kuua mbu.

Simu hiyo ambayo imezinduliwa nchini India inakuja na teknolojia ya mosquito-repelling ultrasonic sound wave ambayo inafanya simu hiyo kuwa kama chanzo cha kufukuza na kuuwa mbu. Hata hivyo simu hiyo ambayo imepangwa kutumika kwa nchini India inakuja ikiwa na sifa za kawaida zifuatazo.

Advertisement

Simu hiyo inakuja na sifa za kawaida za kioo cha inch 5, Ram ya GB 2 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16 pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android Marshmallow. LG imesema kuwa imetoa simu hiyo kama toleo maalumu nchini humo ili kusaidia wananchi wa nchi hiyo kupambana na Mbu.

LG K7i itauzwa kwa pesa ya india Rs 7,990 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 280,000. simu hiyo inategemewa kutumika nchini india na huku ikiwa na kifaa chenye teknolojia hiyo ambacho kipo nyuma ya simu hiyo kama inavyonekana hapo chini.

Bado haija julikana kama simu hii inaweza kutumika sehemu nyingine, kujua zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka.

Chanzo : GSM Arena

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use