Kuongeza Kasi ya Kudownload Kwenye (IDM) Internet Download Manager

Fuata hatua hizi kama unataka kuongeza kasi ya kudownload kwenye programu ya (IDM) au Internet Download Manager
idm idm

IDM au Internet Download Manager ni programu bora ya kudownload ambayo inatumika rasmi kwenye kompyuta. Kutokana na ubora wake programu hii ni moja kati ya programu za muhimu sana kwa karibia kila mtu mwenye kompyuta, umuhimu wake huwa mkubwa zaidi haswa pale unapokuwa unapakua (Download) mara kwa mara vitu mbalimbali kutoka kwenye Internet.

Ukweli ni kwamba programu hii ni muhimu sana kwani siku hizi hakuna mtu mwenye kompyuta ambae hajawahi kudownload kitu kutoka kwenye internet na kama ulisha wahi lazima kwa namna moja ama nyingine utakuwa ulishwahi kutumia programu hii ya (IDM) au Internet Download Manager. Japo kuwa programu hii ni ya muhimu kuna wakati kwenye baadhi ya kompyuta programu ya (IDM) au Internet Download Manager huwa (slow) au taratibu sana kiasi cha mtumiaji kuamua kutumia programu zingine au kukata tamaa kabisa na kuamua kuondoa programu hiyo kutoka kwenye kompyuta yake. Well..! kama wewe ni mmoja wa watu hao makala hii inakuhusu kwani leo tunaenda kujifunza namna ya kuongeza kasi ya kudownload kwenye programu hii ya (IDM) au Internet Download Manager.

Advertisement

Kwa kuanza basi unatakiwa kuwa na vitu viwili vikubwa cha kwanza kabisa hakikisha kompyuta yako inayo programu ya (IDM) au Internet Download Manager kama hauna programu hiyo bofya Hapa kudownload , pili hakikisha unayo bando au (Data) kwenye kompyuta yako kwa kiwango cha chini cha angalau MB 10. Kama utakua na vyote hivyo basi utakuwa umefika nusu ya zoezi hili la kuongeza kasi ya kudownload kwenye programu ya IDM.

Kama utakua umefuata maelezo hayo hapo juu vizuri basi hatua inayofuata ni kudownload programu maalum ambayo itakusaidia kuongeza kasi ya kudownload kwenye programu ya IDM bila wewe kutumia nguvu, wala kuwa na ujuzi wowote wa kompyuta. Ili kudownload programu hiyo bofya kitufe hapo chini.

IDM Optimizer Tool 359 KB

Baada ya kudownload programu hiyo ifungue kutoka kwenye .zip file kisha utakuta programu inayoitwa IDM Optimizer Tool hakikisha una washa programu hiyo kwa kubofya mara mbili kwenye programu hiyo, kisha bofya kitufe cha Maximize Now! baada ya hapo programu hiyo itakuelekeza kubofya kitufe cha kurudia kuiwasha tena programu ya (IDM) au Internet Download Manager, ukimaliza hayo jaribu kudownload file lako au programu yako tena, alafu angalia kama kuna tofauti.

Kama programu hii haitafanya kazi kwako basi usiwe na wasiwasi kwani kuna njia nyingine ambayo unaweza kutumia njia hii ni rahisi sana na unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye programu ya  (IDM) au Internet Download Manager kisha bofya Downloads alafu bofya Options ambayo ipo mwisho kabisa kisha nenda kwenye chumba kilicho andikwa Connection ambacho kipo juu upande wa kulia kisha tafuta mahali palipo andikwa Connection Type/Speed kama unatumia modem chagua sehemu ya mwisho iliyo anza kwa kuandikwa High speed. Baada ya hapo nenda kwenye sehemu uliyo andikwa Max. connection number alfu mbele ya maneno Default max. conn badilisha hiyo namba ambayo mara nyingi hua namba 8 na weka namba ya mwisho kabisa ambayo mara nyingi hua 32 kama unatumia modem, (hapo idm itakuletea meseji ya kuwa kuna baadhi ya server zina kikomo juu ya kiasi cha kuunganisha) bofya OK kisha funga kila kitu alafu jaribu kudownload file lako tena na hapo utaona kasi ya kudownload imeongezeka.

Kama unataka kujifunza haya na mengine mengi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use