Kutumia Programu Mbili kwa Wakati Mmoja Kwenye Simu za Samsung

Inawezekana ulikua haujui lakini hii ndio namna ya kutumia programu mbili kwa wakati mmoja kwenye simu za samsung
samsung-programu samsung-programu

Kama wewe unatumia simu janja (Smartphone) aina ya Samsung basi hii ni kwaajili yako, inawezekana kabisa ulikua hufahamu hili lakini Samsung inayo njia bora ya kukuwezesha kutumia programu mbili kwa wakati mmoja kama jinsi inavyo fanya programu ya Windows 10.

Sehemu hii inapatikana karibia kwenye kila aina ya Simu janja (Smartphone) za Samsung pia ni rahisi sana kuwezesha na haitaji kuwa na programu yoyote kwani sehemu hii inakuja moja kwa moja na simu za Samsung. Kwa wale walio bize sana na simu zao inawezekana kabisa umesha wahi kuona sehemu hiyo lakini kutokana na ubize fulani inawezekana hujawahi kujua sehemu hiyo jinsi inavyofanya kazi.

Kwa kuanza basi kama unatumia simu aina ya Samsung lazima utakua unajua sehemu ya juu kabisa (Notification panel) ambapo ukivuta kwa kwenda chini kuna baadhi ya vibonyezo mbadala (Shortcuts) mbalimbali, sehemu hii pia ukusaidia kusoma meseji mpya kwa haraka bila kwenda kwenye programu yenyewe. Sehemu hii (Notification panel) hua inavyo vibonyezo vyenye maandishi mbalimbali moja kati ya vibonyezo hivyo ni kibonyezo chenye mandishi yaliyo andikwa (Multi window) ili kuwezesha sehemu hiyo hakikisha kibonyezo hicho kinayo rangi ya njano ikiwa na maana sehemu hiyo imewashwa, bila kufanya hivyo sehemu hiyo haitaweza kufanya kazi hivyo ni muhimu kuhakikisha sehemu hiyo imewashwa kabla ya kuendelea.

Advertisement

Kama sehemu hiyo haionekani kwa juu kwenye Simu yako unaweza kuipata kwa kubofya (Settings) kisha bofya (Display), kumbuka Display hupatikana kwenye sehemu tofauti kila simu kwa mfano kwenye Samsung Galaxy S4 sehemu hii hupatikana kwenye (Settings – My Device – Display). Kama umesha fanikiwa kuona sehemu hiyo tafuta na weka tiki kwenye chumba chenye maneno (Multi window).

Baada ya hapo sasa unaweza kuanza kutumia sehemu hiyo inayopatikana kwenye simu yako ya Samsung, basi ili kuanza kutumia bofya kwa muda mshale uliojikunja (Back Button) ulioko kulia chini kwenye simu yako, kisha utaona upande wa kulia kumefunguka programu mbalimbali zilizoko kwenye simu yako, bofya moja ya programu kisha baada ya programu kufunguka bofya tena mshale uliojikunja (Back Button) ulioko kulia chini kisha utaona tena programu zimefunguaka kisha bofya tena programu nyingine na hapo utaona programu hizo zimejigawa nusu kwa nusu kwenye kioo cha simu yako.

Kwa kufanya hayo yote hapo juu utakua umewezesha simu yako ya Samsung kutumia programu mbili kwa wakati mmoja, kumbuka unaweza kutumia programu zozote zilizoko hapo juu au unaweza kubadilisha nyingine kwa kurudia hatua hizo hapo juu. ili kutoka kwenye sehemu hiyo unaweza kubofya kibonyezo cha katikati yani (Home button).

Bila shaka utakua umeweza kutumia programu mbili kwa wakati mmoja kwenye zimu yako ya Samsung. Kama unataka kujifunza haya na mengine mengi kuhusu teknolojia endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use