Jinsi ya Kujua Nani Anae Angalia Sana Akaunti Yako ya Facebook

Kama unataka kujua nani amekua akiangalia sana akaunti yako ya facebook basi fuata hatua hizi rahisi
Jinsi ya Kujua Nani Anae Angalia Sana Akaunti Yako ya Facebook Jinsi ya Kujua Nani Anae Angalia Sana Akaunti Yako ya Facebook

Kuna wakati unakuta unataka kujua ni nani anae angalia sana akaunti yako ya facebook, iwe wewe ni admin wa page, group au hata akaunti binafsi nadhani lazima utakua anatamani sana kujua ninani amekua mfuatiaji mzuri wa profile, group au hata page yako. Basi kama wewe ulikua unatamani kujua hilo basi usiwe na wasiwasi leo Tanzania tech tunakuletea njia rahisi sana na salama ya kujua ni nani amekua akitembelea profile, page au group lako mara kwa mara.

Kwa kuanza basi kumbuka ni lazima uwe wewe ndio mwenye akaunti hiyo ya Facebook kwani bila hivyo hutoweza kufanikisha hatua hizi, kwa maneno mengine ni kwamba ni lazima uwe umeingia (ume-login) kwenye akaunti yako hiyo unayotaka kujua nani amekua akitembelea mara kwa mara. Pia ni muhimu kujua kuwa ili uweze kufanya hatua hizi unatakiwa uwe umeingia (ume-login) kwenye akaunti yako hiyo kwa kutumia kompyuta iwe ni laptop au desktop.

Baada ya kuhakikisha hayo yote hapo juu basi twende moja kwa moja tukaangale jinsi ya kuangalia nani anae angalia sana akaunti yako ya facebook. Kwa kuanza ingia kwenye akaunti yako ya facebook kisha bofya kwenye profile yako au page au group unalotaka kujua nani amekua anatembelea sana, baada ya hapo hakikisha page hiyo au akaunti yako imemaliza kusoma (kuload) vizuri kisha futa hatua hizo hapo chini.

Advertisement

Kwenye Keyboard ya kompyuta yako (laptop au desktop) bofya vibonyezo Ctrl pamoja na U kwa pamoja yaani (Ctrl+U) au unaweza kutumia Mouse ya kompyuta yako kwa kubofya kibonyezo cha Mouse cha upande wa kulia (Right Click) kisha chagua sehemu iliyoandikwa view page source hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye page yenye code za akaunti yako. Subiri page hiyo imalize kusoma (ku-load) kisha bofya tena kwenye keyboard yako Ctrl pamoja na F (Ctrl+F) ukiwa kwenye page hiyo yenye code za akaunti yako.

Baada ya hapo utaona kwenye kioo chako box limefunguka upande wa kulia juu copy hizo code hapo chini (kucopy bofya view raw) kisha weka (paste) kwenye box hilo na bofya Enter kwenye keyboard yako.

Baada ya hapo utaona namba nyingi zikianza mbele ya maneno hayo baada ya neno List, namba hizo zinakuwa na tarakimu 15 copy namba hizo kisha andika www.facebook.com/ kwenye sehemu ya kuandika link kwenye browser yako kisha weka namba hizo 15 mbele ya mkato yani www.facebook.com/123456789012345 kisha bofya Enter kwenye keyboard yako.

Baada ya hapo utaona (profile) akaunti ya mtu ambae ndio anatembelea sana profile page yako kwenye mtandao wa facebook, kumbuka namba ya kwanza ndio inayo wakilisha anaetembelea sana kama ukiangalia namba hizo ziko nyingi inamaanisha zimejipanga kwa mtu wa kwanza mpka wa mwisho, kama unataka kujifunza zaidi angalia video hapo chini.

Kama umekwama mahali popote usisite kuuliza kwenye maoni hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use