Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua

Hizi ndio njia mtu anazoweza kutumia kusoma SMS bila wewe kujua
Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua

Kabla ya kuanza makala hii ningependa kutoa angalizo kuwa njia hii ni kwa ajili ya kujifunza na imelenga kusaidia kujua mbinu anazo weza kutumia mtu yoyote kusoma meseji zako bila wewe kujua. Pia kumbuka kuwa njia hizi ni sio udukuaji bali hizi ni huduma ambazo zina tolewa na tovuti na kampuni mbalimbali ambazo zinapatikana mtandaoni. Kumbuka ni kinyume na sheria za nchi kuweka programu yoyote kwenye simu ambayo hauna mamlaka nayo kutumia kwa asilimia 100.

Kwa kusema hayo inakupasa kuhakikisha hautumi vibaya kwa namna yoyote makala hii au makala nyingine zozote zilizopo kwenye tovuti hii.

Basi baada ya hilo sasa twende kwenye makala yetu moja kwa moja, Kama kwa namna yoyote unahisi kuna mtu anasoma meseji zako bila wewe kujua basi hakikisha unasoma makala hii hadi mwisho kwani nitaenda kukwambia njia rahisi ya kujua kama kuna mtu anasoma meseji zako bila wewe kujua.

Advertisement

Spyhuman

Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua

Tovuti ya kwanza kwenye list hii ni spyhuman, tovuti hii inakupa uwezo zaidi ya kusoma meseji za mtu kwani hii inauwezo wa kuruhusu kusoma meseji za whatsapp na mitandao mingine ya kijamii, pia utaweza kusoma call log ikiwa pamoja na uwezo wa kujua namba inayopigwa zaidi kwenye simu ya mtu husika. Mbali na hayo tovuti hii inakuja na uwezo wa kuzuia mtu husika kutumia baadhi ya programu kwenye simu yake pamoja na mambo mengi. Tovuti hii inakuja na vifurushi vya bure na vifurushi vya kulipia ambavyo unaweza kutumia kufanya mambo mengi zaidi.

Tembela Tovuti Hapa

Mobile Tracker Free

Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua

Mobile Tracker Free ni tovuti nyingine ambayo inaweza kusaidia kusoma meseji za mtu bila yeye kujua, tovuti hii ni kama tovuti iliyopita na inakupa uwezo wa zaidi ya kusoma meseji za mtu. Kupitia tovuti hii utaweza kurekodi simu za mtu anazopigiwa, utaweza kujua app gani anatumia zaidi pia utaweza kujua meseji zake anazotuma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, na mambo mengine mengi. Uzuri wa tovuti hii ni bure kabisa halipii kitu chochote.

Tembela Tovuti Hapa

Spapp Monitoring

Jinsi ya Kujua Mtu Anaesoma SMS Zako Bila Wewe Kujua

Tovuti nyingine ambayo inaweza kusaidia kusoma meseji za mtu mwingine ni Spapp Monitoring, tovuti hii haina tofauti na tovuti zilizo tangulia. Kupitia tovuti hii utaweza kusoma meseji za mitandao ya kijamii, kujua namba inayo pigwa zaidi ikiwa pamoja na mambo mengine mengi. Kupitia tovuti hii utaweza kupata muda wa bure wa kutumia tovuti hiyo na baada ya hapo unatakiwa kulipia hudumu hiyo.

Tembela Tovuti Hapa

Kujua Kama Mtu Anasoma Meseji Zako Bila Wewe Kujua

Sasa twende moja kwa moja kwenye njia ambazo unaweza kujua kama mtu anasoma meseji zako bila kujua. Kumbuka hakuna njia maalum ambayo unaweza kujua moja kwa moja bali inakuhitaji kufanya njia hizi zote ili kuwa na uhakika zaidi.

Weka Anti Virus ya Kaspersky Mobile

Anti virus ya Kaspersky Mobile ni moja kati ya App ambayo inafanya kazi vizuri sana ya kuweza kulinda simu yako dhidi ya virus pamoja na programu mbalimbali ambazo zinaweza kumsaidia mtu kusoma meseji bila wewe kujua. App ya Kasperky itakusaidia kulinda mtu asiweke app yoyote kwenye simu yako ambayo itakuwa na uwezo wa kudukua simu yako kwa namna yoyote. Unaweza kupakua app ya Kaspersky Mobile hapo chini.

Download App Hapa

Pendelea Kuzima Internet Baada ya Kutumia

Mara nyingi huduma kama hizi huwa zinatumia internet kuweza kupakia data kwenye server ambazo ndio zinatumiwa na mtu kuweza kuona meseji zako, hivyo basi kama unaona data zinaisha haraka bila hata wewe kutumia au simu yako inachukua mda mrefu kufanyakazi hasa kwenye sehemu ya meseji za kawaida na WhatsApp basi huwenda njia kama hii inatumika kusoma meseji zako bila wewe kujua.

Angalia Alama Uzizo zijua Sehemu ya Notification

Mara nyingi kwenye sehemu ile ya ujumbe inayopatikana juu kwenye simu yako huwa inaonyesha kama simu yako inatumia app ambayo ina ruhusu programu ambazo ni za hatari, ujumbe huo ni ishara ya kuwa kuna programu ambayo inaweza kutumia data zako za siri kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye tovuti mbalimbali ni muhimu sana kuwa makini na sehemu hii.

Angalia sehemu ya Accessibility

Mara nyingi app hizi zenye uwezo wa kutuma data zako za siri huwa na ulazima wa kuruhusiwa kwenye simu yako kupitia sehemu ya Accessibility, sehemu hii inapatikana kwenye simu zote za Android na unaweza kuipata kupitia Settings > Accessibility kisha angalia sehemu ya Services ambayo huwa inapatikana mwisho kabisa wa ukurasa huo.

Angalia majina ya apps ambazo zinatumia sehemu hiyo kama kuna app yoyote ambayo hukuweka wewe basi bila shaka kuna mtu anasoma meseji zako bila wewe kujua. Mara nyingi sehemu hii haitumiki na apps nyingi hivyo kama ukikuta inatumika na app yoyote basi ni vizuri kuzima kwanza app hiyo kisha angalia kama kuna tatizo lolote kwenye simu yako. Hii ni muhimu kwani mara nyingi majina ya apps hizi yanakuwa tofauti na unaweza usijue kama ni app ya kusoma meseji zako bila wewe kujua.

Na hizo ndio njia ambazo unaweza kuzitumia kujua kama mtu anasoma meseji zako bila kujua, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kutembelea ukurasa wetu wa maujanja na utaweza kujifunza mambo mengi zaidi. Pia usisahau ku-subscribe kwenye channel yetu kwani wiki hii tunategemea kufanya muendelezo wa awamu ya pili ya njia ya kutengeneza tovuti kwa kutumia simu ya mkononi.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use