Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Hizi Hapa Apps Nzuri za Kusaidia Kujua Mahali Mtu Alipo

Utaweza kujua mahali mtu alipo kabisa kwa kuangalia kwenye ramani
Hizi Hapa Apps Nzuri za Kusaidia Kujua Mahali Mtu Alipo Hizi Hapa Apps Nzuri za Kusaidia Kujua Mahali Mtu Alipo

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamekuja kusoma makala hii ukijua kuwa utakutana na app zitakazo kusaidia kujua mahali mpenzi wako alipo bila yeye kujua, basi pengine naomba nikuombe samahani. Kwani kupitia makala hii tutazungumzia app ambazo zitakusaidia kujua mahali mtu alipo huku na yeye akiwa anajua kuwa amekuruhusu ujue mahali alipo.

Makala hii inalenga zaidi familia na watu wa karibu ambao pengine ungependa kujua walipo ili kuhakikisha usalama wao kwa namna moja ama nyingine, pia kwa wazazi ambao wameanza kuruhusu matumizi ya smartphone kwa watoto wao pengine hii ni njia bora ya kujua mwanao alipo muda wote utakapo kuwa unahitaji. Basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja tungalie apps hizi nzuri.

Advertisement

Life360 ni app nzuri sana kwajili ya kujua mahali mtu alipo, app hii imelenga famili na inakuja na sehemu nyingi nzuri zitakazo kusaidia kujua usalama wa mtu wa karibu yako kwa wakati wote hata kama uko mbali na yeye. Kupitia app hii utaweza kujua mtu alipo kupitia ramani huku pia ukipata ruhusa ya kuangali vitu mbalimbali kama mwendo anao tembea au kuendesha gari pamoja na mambo mengine mengi, app hii ni bora sana kama unataka kulinda familia yako.

Find My Friends
Price: Free+

Find My Friends ni app nyingine nzuri ambayo inaweza kukusaidia kujua mtu alipo, app hii inakuja na sehemu nzuri ambazo zinakusaidia kushiriki mahali ulipo na mtu wako wa karibu. App hii inakuja na sehemu nyingine nyingi kama sehemu ya kuchat na ndugu na jamaa walio kwenye ramani pamoja na sehemu nyingine nyingi.

Family Locator ni app nyingine nzuri sana ambayo inakusaidia kujua mtu alipo kwa urahisi, tofauti na app nyingine ambazo zimetangulia app hii yenyewe ina uwezo wa kushiriki mahali ulipo pale utakapo bofya kitufe cha kuomba msaada, hii inasaidia sana kama wewe au mtu mmoja wa familia yako yupo kwenye matatizo na yupo sehemu asiyo ijua.

Zoemob Family Locator
Price: Free

Zoemob ni app nyingine nzuri sana ambayo inakusaidia sana kuweza kuja mwana familia au ndugu na jamaa walipo, app hii itakusaidia sana pale unapota kujua amahali mtu anapo enda ikiwa pamoja na kupata taarifa kama amafika, mbali ya hayo app hii pia inakupa uwezo wa kuchat na ndugu na jamaa kwa urahisi na bila gharama yoyote.

Glympse ni app nyingine maarufu ambayo inaweza kukusaidia kujua mtu alipo pamoja na mambo mengine mengi. App hii inakupa uwezo wa kujua mahali kwenye matamasha mbalimbali ikiwa pamoja na sherehe mbalimbali ambazo zimeandaliwa na ndugu au jamaa zako wa karibu.

My Family ni app nyingine nzuri sana ambayo inaweza kusaidia sana hata wale wenye wivu kidogo wa mapenzi, tofauti ya app hii na nyingine zote kwenye list hii ni kuwa, kupitia app hii pia utaweza kuangalia data mbalimbali za mtu wako wa karibu, kama vile tovuti alizo tembelea kwenye kivinjari cha simu yake pamoja na mambo mengine mengi, kama wewe una wivu wa mapenzi basi hebu jaribu sasa app hii pengine inaweza kukusaidia… ila acha wivu wewe…!

Mambo yanazidi kuwa mazuri kwa wenye wivu wa mapenzi, app hii ya All Tracker Family ni tofauti na app nyingine kwenye list hii kwani app hii itakusaidia kujua mahali mtu alipo ikiwa pamoja na uwezo wa kuona meseji SMS za mtu wako wa karibu pamoja na kuangalia Call Log au watu walio mpigia au walio mpigia… nzuri ehhh… umeona eh.. hii inakufaa sana mtu wangu hebu jaribu hii sasa.

Find My Devices
Price: Free+

Kwa hii ya mwisho nadhani ni bora zaidi kwa wale ambao wanataka kujua zaidi kwa kutumia video yaani kwa kupata ushahidi kabisa wa video pamoja na kujua mahali mtu alipo kwa urahisi app hii ni nzuri sana, kwa sababu unapenda video hebu angalia video hapo chini jinsi app hii inavyo fanya kazi, na uhakika kabisa utaipenda hii…

Mpaka siku nyingine natumaini app hizi zinaweza kukusaidia kujua mahali mtu alipo, kama unataka app nyingine nzuri zaidi basi hakikisha unasoma hapa kujua app nzuri za kukusaidia wewe ambae unatafuta ajira rasmi. Mpaka siku nyingine endelea kutembelea Tanzania Tech.

1 comments
  1. sa mbona hujasema inafanyaje kazi na niki download kwangu pekeyake imetosha ama na kwa victims ebu ongeza nyama

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use