Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya Explore (Android na iOS)

Application za YouTube za Android na iOS zimeboreshwa zaidi
YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya Explore (Android na iOS) YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya Explore (Android na iOS)

Baada ya majaribio ya muda mrefu hatimaye YouTube imetangaza ujio wa sehemu mpya ya Explore, sehemu hii mpya itakuwa badala ya sehemu ya Trending ambayo ina kuwepo ndani ya apps zote za YouTube za Android pamoja na iOS..

Kwa mujibu wa YouTube, sehemu hiyo mpya ya Explore inakuja ikiwa imeboreshwa zaidi na itakuwa ya tofauti zaidi na rahisi kutumia. Sehemu hiyo itakuwa na shortcuts kwenda kwenye vipengele muhimu kama Gaming, Music, Fashion & Beauty, Learning, na sehemu nyingine mbalimbali. Kama upo tanzania, kwa sasa kupitia sehemu hiyo unaweza kuona sehemu mbili za Top 100 Music, pamoja na Gaming.

Advertisement

YouTube Yaja na Sehemu Mpya ya Explore (Android na iOS)Sehemu ya Trending, nayo imeamishiwa ndani ya sehemu ya Explore ambapo pia utaendelea kuona video zilizo Trending kwa siku kupitia ukurasa huo. Kwa mujibu wa YouTube sehemu hii tayari inaonekana kwa watumiaji wote wa Android na iOS na unaweza kuona sehemu hii sasa ndani ya App hiyo.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu YouTube unaweza kusoma hapa kujua mapato ya mtandao wa YouTube kwa mwaka 2019. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi kuhusu habari mpya za teknolojia kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use