Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps Nzuri za Kusaidia Kuficha SMS Kwenye Simu ya Android

Njia bora za kukusaidia kuficha SMS kwenye simu yako ya Android
Apps Nzuri za Kusaidia Kuficha SMS Kwenye Simu ya Android Apps Nzuri za Kusaidia Kuficha SMS Kwenye Simu ya Android

Kama wewe ni mmoja wa watu wanao pendelea “kuficha ficha” basi na hakika unafurahia makala za Tanzania Tech.., hapo jana tumeongelea jinsi ya kusoma meseji za WhatsApp bila mtu kujua kama upo online na leo tunaongelea jinsi ya kuficha SMS kwenye simu ya Android.

Anyway.. hii yote ni kati hali ya kujifunza mambo mbalimbali kwani huwezi kujua utahitaji kutumia njia hizi wakati gani. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye list hii ya apps nzuri kwa ajili ya kuficha SMS kupitia simu yako ya mfumo wa Android. Kumbuka list hii haijapangwa hivyo apps zote kwenye list hii ni nzuri.

Advertisement

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye uhitaji wa haraka wa kuficha SMS pamoja na mambo mengine mengi basi app ya Vault ni nzuri sana kwako. App hii ina uwezo mkubwa wa kuficha vitu mbalimbali zaidi ya SMS kwenye simu yako huku ikikupa ulinzi bora kwenye programu nyingine kama Facebook, Messenger, WhatsApp na nyingine kama hizo.

App nyingine ambayo ni bora hasa kwenye kuficha SMS ni app ya Message Locker, app hii ina uwezo mkubwa wa kuficha SMS ikiwa pamoja na kuweka password kwenye app mbalimbali zinazokuja na simu yako. Unaweza kuweka password kwenye sehemu ya SMS, Email pamoja na sehemu nyingine mbalimbali ndani ya simu yako ya Android.

Kama unataka kufanya zaidi ya kuficha SMS basi app hii ya Private Message Box ni msaada mkubwa kwako. App hii inao uwezo wa kuficha SMS kwa kutumia password lakini pia inakuja na sehemu ambayo unaweza kuficha Call Log za namba maalum, kwa kutumia app hii unaweza kuhifadhi namba ambayo ukipigiwa haionyeshi popote kama ulipigiwa.

App nyingine ambayo ni bora sana kuwa nayo ni pamoja na app ya Calculator Pro+. App hii kama ilivyo jina lake inaonekana kama kikokotozi au Calculator, lakini ndani yake inakuja na sehemu ya siri ya kuchat na namba ambazo SMS zake hutaki zionekane na mtu yoyote. Kupitia app hii utaweza kuwaka namba ambayo utaki meseji zake zionekane na kila wakati hiyo namba inapo tuma SMS basi SMS hizo hazito onekana kwenye app ya kawaida ya ujumbe mfupi kwenye simu yako na badala yake zita ondolewa na kupelekwa ndani ya app hiyo.

Na hizo ndio app nilizo kuandalia kwa siku ya leo ambazo zitakusaidia kuweza kuficha SMS kupitia simu yako ya Android. Kama unataka kuangalia njia nyingine ya kuficha SMS pamoja na Call Logs unaweza kusoma hapa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube Hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use