Sasa Utaweza Kuwasha Muonekano wa Giza Kupitia Play Store

Jifunze hatua kwa hatua jinsi ya kuwasha sehemu hiyo.
Sasa Utaweza Kuwasha Muonekano wa Giza Kupitia Play Store Sasa Utaweza Kuwasha Muonekano wa Giza Kupitia Play Store

Muonekano wa giza au (Dark Mode) ni moja ya trends za mwaka 2019 kuja mwaka 2020, programu nyingi sana pamoja na mifumo ya uendeshaji ya Android, Mac, Windows na iOS yote sasa inakuja na uwezo wa kuwasha muonekano wa giza au Dark Mode kwa urahisi kabisa.

Lakini kama haitoshi baada ya Facebook kuwezesha sehemu hiyo kupitia programu yake ya WhatsApp, hatimaye sasa Google nayo imeamua kuongeza sehemu hiyo ya Dark Mode kupitia soko lake la Play Store. Kwa mujibu wa tweet kupitia akaunti ya Google Play kwenye mtandao wa Twitter, Play Store sasa itakuwa na sehemu maalum ya kuwasha na kuzima muonekano huo wa giza bila kujali aina ya simu mtumiaji anayo tumia.

Kama unavyoweza kuona kwenye video ya hapo juu, ili kuwasha muonekano huo wa giza unatakiwa kufungua app ya Play Store, kisha bofya vimistari vya menu upande wa kushoto juu, baada ya menu kufunguka bofya Settings kisha tafuta Theme kweli list ya Settings kisha chagua Dark kuwasha muonekano wa giza moja kwa moja.

Sehemu nyingine iliyopo kwenye Menu hiyo ni sehemu ya “Set by Battery Saver” sehemu ambayo itakusaidia kuwasha muonekano wa giza automatic pale simu yako inapo pungua chaji sana.

Kwa sasa sehemu hii tayari inapatikana kwa watumiaji wote wa simu za Android na unaweza kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja kwa kufuata hatua hapo juu. Kama unataka kujua jinsi ya kuwasha muonekano huu kwenye programu ya WhatsApp basi unaweza kusoma hapa, lakini kama unataka kuwasha muonekano wa giza kwenye programu ya Instagram basi soma makala hii hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use