Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Mtu hatoweza kuona jina lako pale anapokuwa hana namba yako kwenye simu yake
Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi ni wazi kuwa unayo au ulishawahi kujaribu app ya Truecaller kwenye simu yako. Kama ufahamu kuhusu app hii, basi pengine ni kwambie kuwa Truecaller ni app inayo kusaidia kujua nani anaekupigia simu hata kama huna namba yake kwenye phonebook ya simu yako.

Hadi mwaka jana, app hii inayo watumiaji zaidi ya milioni 250 duniani kote huku watumiaji wapya wakizidi kuongezeka kila siku. Lakini pamoja na kuwa app hii ni maarufu kuna wakati unahitaji ufaragha pale unapo amua kumpigia mtu simu na hutaki kila mtu mwenye app hii aweze kujua kuhusu wewe.

Advertisement

Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kuzuia mtu kuona jina lako pale unapo piga simu kwenye simu yake akiwa na app ya truecaller na kama hana namba yako kwenye simu yake. Kumbuka njia hii inahitaji uwe ulishawahi kutumia app ya Truecaller na kama ulisha futa app hii kwenye simu yako basi ni lazima kurudisha app hiyo ili uweze kufanya hatua hizi kikamilifu.

Basi kwa kuanza ingia kwenye app ya Truecaller kisha fungua app hiyo na bofya Menu iliyopo juu upande wa kushoto.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya hapo kwenye list chagua sehemu ya settings iliyopo chini mwisho kabisa.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya hapo moja kwa moja utafunguka ukurasa mwingine na moja kwa moja shuka mpaka mwisho wa ukurasa huo kisha chagua Privacy Center.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya kubofya sehemu hiyo utafunguka ukurasa mwingine, moja kwa moja shuka mpaka chini kisha chagua sehemu ya ‘Deactivate’.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya kubofya hapo utaletewa maandishi ya kuthibitsha, moja kwa moja bofya sehemu ya OK kuweza kuthibitisha. Kumbuka kwa kufanya hivyo utakuwa umezima namba yako kutumika kwenye Truecaller.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea kwenye hatua za kuondoa namba yako isiweze kuonekana jina pale utakapo mpigia mtu ambaye hana namba yako kwenye simu yake.

Kitu cha msingi hakikisha unatembelea link hapo chini, link hiyo utakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa ambao utaweza kuondoa namba yako kwenye data kazi ya truecaller. Kumbuka ni muhimu kupitia hatua hapo juu kabla ya kufanya hatua hii.

Tembela Tovuti Hapa

Baada ya kutembelea tovuti hapo juu, moja kwa moja andika namba yako kwa usahihi kwenye chumba kilichowazi, hakikisha unaanza na namba za utambulisho wa nchi uliyopo. Kwa Tanzania hakikisha una anza na +255 kisha andika namba yako bila kuandika sifuri.

Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuona Jina Lako Kwenye Truecaller

Baada ya hapo bofya kutufe cha I’m not a robot kisha malizia kwa kubofya sehemu ya Unlist Phone Number iliyopo mwisho kabisa wa ukurasa kama inavyo onekana kwenye picha hapo juu.

Kama ulifuata hatua zote toka mwanzo basi moja kwa moja namba yako itaweza kuondolewa na mtu hatoweza kuona jina lako pale unapo mpigia simu kama hana namba yako kwenye phonebook yake. Kumbuka baada ya kufuata hatua hizi inaweza kuchukua hadi masaa 24 hadi namba yako kufutwa kabisa kwenye datakazi ya Truecaller.

Natumaini utakuwa umeweza kuzuia mtu kuona jina lako kwenye app ya Truecaller, kama unataka kijifunza zaidi hakikisha unasoma hapa kujua jinsi ya kutumia app ya Truecaller bure kabisa bila kulipia. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use