Inawezekana kwa namna yoyote ukawa na uhitaji wa kupiga simu au kutuma meseji nje ya nchi na huna salio la kutosha kuweka kwenye simu yako kuweza kuwapigia ndugu na jamaa waliopo ughaibuni. Kupitia maujanja haya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kupiga simu na kutuma meseji nje ya nchi bure kabisa.
Kwa kuanza unahitaji vitu kadhaa, kitu cha kwanza cha muhimu ni Internet unahitaji angalau kiasi cha MB 200 na kuendelea pia unatakiwa kuwa na akaunti ya Facebook au Google. Kama unavyo vitu vyote hivi basi unaweza kuendelea hatua inayofuata.
Hatua ya kwanza kama unatumia Android Download App ya Yalp Store kisha install kwenye simu yako vizuri kabisa, App hii hapo Play Store hivi ni muhimu kudownload kupitia Link hapo juu. Kimsingi app hii ina umuhimu kwenye maujanja haya kwani itakusaidia kuweza kudownload app ambazo zimezuiliwa kwa Tanzania. Baada ya kudownload app hiyo endelea kwa kufuata hatua hizi.
Application zote zilizotajwa kwenye video hii link hizi hapa chini unaweza kubofya hapo kwaajili ya kupakua app hizi. Njia hii ni nzuri sana Guys kwani inaweza hata kukusaidia kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki endapo nao pia watafuata njia hii.
nikiidonload naambiwa this item isn’t available in your country.hapo cjui shida ni cm yangu ama vp
Angalia video, pia ndio sababu ya kudownload App ya Yalp Store
Nimependa xaxa elmu ya humu tunaomba kila sku muwe mnatuma habari mpya Mna tunajifunza xnaaa
Betrida Msamba 20 days ago
je mngeonaje mfundishe sanaa
nipenda hiyoo happ
Sijaelewa kitu hapo.. Hii namba ni kwa USA na Canada tu au hata nchi za Africa inafanya kazi..?
Unaposema ni kwa USA na Canada Tu una maana gani.?
Nimefanya kama hivyo ila nikituma msg kwa mtu ambae yuko kenya inaferi
Maoni*nmekipenda sana elimu yenu …lakini naomba pia kupata elimu ya jinsi ya kuhack chat za mtu mwingine za watsup ambaye ako mbali na mimi .shkuraniii nyotee
Nimesha download app hiyo Yalp lkn bado nikijaribu kuidownload text now inagoma na hapo nimeweka kuipata kupitia Yalp bado inagoma
Mbona inafanya kazi kama kawaida, unatumia simu ya aina gani.
Natakiwa kutumia simu ya aina gani
Simu yako ya kawaida.
Jaman nipo omani nataka niwe natumia line yangu ya Tanzania kuunganishwa MB nifanyaje hadi mtu wa tanzania awe ananiunganisha na Mb za hk