Jinsi ya Kutuma Meseji za WhatsApp Bila Kushika Simu

Kama unataka kutuma meseji za WhatsApp kwa muda maalum bila kushika simu soma hii
Jinsi ya Kutuma Meseji za WhatsApp Bila Kushika Simu Jinsi ya Kutuma Meseji za WhatsApp Bila Kushika Simu

Ni kweli kuwa biashara nyingi siku hizi zina hamia mtandaoni, hii ni kutokana na urahisi wa mawasiliano unaoletwa na teknolojia. Lakini ni wazi kuwa kama binadamu sio kila mara unaweza kuwa na simu yako mkononi ukiwa tayari kuchat na wateja.

Kuliona hili nimekuletea apps nzuri ambazo zinaweza kukusaidia sana kujibu meseji za WhatsApp za wateja wako bila wewe kufungua simu yako au kujibu meseji hizo wewe binafsi.

Kupitia makala hii utaweza kupata njia ambazo zitakusaidia kujibu maswali ya muhimu ya wateja wako ikiwa pamoja na kuendelea kufanya kazi hata kama hujashika simu yako mkononi, basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende tukangalie njia hizi nzuri.

Advertisement

SKEDit Scheduling

SKEDit ni app nzuri sana ya Android ambayo inakusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe, mbali ya WhatsApp app hii inaweza kufanya mambo mengi sana kama vile kusaidia status kwenye mtandao wa Facebook zijiposti zenyewe, kusaidia barua pepe ijitume yenyewe pamoja na meseji za kawaida SMS nazo unaweza kufanya zijitume zenyewe kupitia App hii.

Download Hapa

AutoResponder for WA

AutoResponder for WA ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya kusaidia meseji za WhatsApp kujituma zenyewe, app hii ni nzuri sana kwa sababu hii inakusaidia kujibu meseji za watu bila hata wewe kuangaika kufungua app ya WhatsApp. App hii inauwezo wa kusoma maneno kadhaa ambayo utakuwa umeyaandika ndani ya app hiyo na pale mtu atakapo andika maneno hayo kama ujumbe wa WhatsApp basi atapata majibu ambayo umeandika awali.

Download Hapa

WhatsAuto – Reply App

Whatauto - Auto Reply

WhatsAuto ni app nyingine ambayo haina tofauti sana app iliyopita, app hii nayo itakusaidia kujibu watu meseji pale watakapo kuwa wamekuandikia ujumbe fulani kwenye WhatsApp. Kumbuka ni lazima kuandika sentensi ambayo unataka ijibiwe kwa kutumia app.

Download Hapa

Autoresponder for WA Auto-reply SMS Business Card

Autoresponder for WA Auto-reply SMS Business Card ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa simu za Android, app hii nzuri kwa sababu inakusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe lakini pia inakusaidia kutuma Business Card kupitia SMS app hii ni nzuri sana kwa wafanya biashara hivyo kama wewe ni mfanya biashara nakushauri jaribu app hii.

Download Hapa

AutoResponder for FB Messenger

App ya mwisho kwenye list hii na tofauti kidogo kwani haiusiani na WhatsApp, App hii itakusaidia sana kama wewe ni mtumiaji wa Facebook Messenger. Utaweza kuwajibu watu meseji zako kwa haraka kupitia Facebook Pia utaweza kufanya meseji hizo zijitume zenyewe bila wewe kufungua app ya Messenger.

Download Hapa

Na hizo ndio apps nzuri ambazo zinaweza kusaidia kufanya meseji za WhatsApp zijitume zenyewe, kumbuka app hizi ni kwa ajili ya Android na kama unatumia mfumo wa iOS basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuja na list ya App hizo kwa mfumo huo. Kama unataka kujua apps nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua App za kusaidia kutengeneza Beat kupitia simu yako ya Mkononi ya Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use