Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako

Washa Tochi, Zima Simu, Fungua App, Play Muziki na Mengine Mengi
Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android njia hii inakuhusu, kupitia njia hii nitaenda kuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kubadilisha sehemu ya kamera ya mbele kuwa kitufe maalaum, yaani kama simu yako ina muonekano kama picha hapo chini basi njia hii ni kwaajili yako.

Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako

Haijalishi sehemu hiyo ya kamera ina kamera mbili au kamera mmoja bali kama kamera ya simu yako ipo ndani ya kioo njia hii itaenda kufanya kazi kwenye simu yako.

Advertisement

Sasa kitu cha muhimu ni kuhakikisha unapakua app kupitia link hapo chini, app hii itakusadia kuweza kubadilisha sehemu hiyo na kuruhusu sehemu hiyo kutumika kama kitufe maalum.

Yaani utaweza kuwasha kamera, kufungua app maalum, kuwasha tochi na mambo mengine mengi moja kwa moja kwa kugusa sehemu hii kwenye simu yako.

Touch The Notch
Price: Free

Pakua Toleo la Bila Kununua

Baada ya kupakua app hii moja kwa moja fungua app hii na kisha ruhusu app hii kwenye permission mbalimbali kisha utapelekwa kwenye uwanya wa Settings.

Fanya Haya kwa Kugusa Sehemu ya Kamera Kwenye Simu Yako

Unaweza kufanya mambo mbalimbali kama unaweza kuona kwenye video hapo chini, hakikisha unajaribu Menu mbalimbali ili kujua menu gani ni muhimu kwako.

Unaweza kufanya yote hayo kwa kubofya tu sehemu ya kamera kwenye simu yako. Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitia maoni hapo chini, pia kwa unataka kujua maujanja zaidi unaweza kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use