Jinsi ya Kuzuia Mtu Kuhack Instagram, Facebook na Twitter

Kuzuia akaunti zako za mitandao ya kijamii kudukuliwa (Kuhackiwa)
kuzuia kuhack facebook, tweitter na instagram kuzuia kuhack facebook, tweitter na instagram

Katika hali ya kawaida kila siku watu wamekuwa waki lalamika kuhusu akaunti zao za biashara au za kawaida kudukuliwa. Lakini ni vyema ujue kuwa mitandao hiyo ina namna ya kuzuia au kukujulisha pindi mtu atakapo taka kufanya udukuzi kwenye akaunti yako. Leo Tanzania tech tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka ulinzi na kuzuia akaunti hizo za mitandao ya kijamii kuhackiwa. Bila kupoteza muda twende zetu…

  • Jinsi ya Kuzuia Akaunti ya Twitter Kuhackiwa (Kompyuta)

Kwa kuanza ingia kwenye akaunti yako ya twitter kisha bofya kwenye picha yako ya profile, kama unatumia kompyuta kisha Settings and Privacy, baada ya hapo utaona chini kidogo kumeandikwa Securty na chini yake kumeandikwa Login verification.

Advertisement

Kwa mbele utaona kichumba kimeandikwa Verify login requests bofya hapo kisha hakiki akaunti yako kwa kuingiza password kisha bofya Start, kufikia hapo unatakiwa uwe umeweka namba yako ya simu kwenye akaunti yako kama hujaweka sehemu hii haitafanya kazi.

Kama hujaweka namba weka namba kisha endelea kwa kubofya Send hapo utatumiwa namba za uthibitisho kwenye simu yako kisha andika namba hizo kwenye kichumba hicho kisha bofya Verify, baada ya hapo utapewa backup code ambazo hizi ni muhimu kama umeibiwa simu au umepoteza line yako.

Hifadhi code hizo mahali kwa kuziandika na zitunze kwani bila hizo kama line au simu imepotea hutoweza kuingia kwenye akaunti yako. Mpaka hapo kila mara utakapo ingia kweye akaunti yako ya Twitter namba maalum zitatumwa kwenye simu yako na unatakiwa kuingiza namba hizo kwenye akaunti yako ili kuweza kuingia au kulogin kwenye uwanja wako wa Twitter.

  • Jinsi ya Kuzuia Akaunti ya Twitter Kuhackiwa (Simu)

Ingia kwenye programu yako ya Twitter kisha bofya picha yako ya Profile kisha bofya Settings and privacy kisha bofya Account kisha bofya Security hapo weka tiki mahali palipo andikwa Login Verification, thibitisha akaunti yako kwa kuweka password yako kisha bofya start kisha bofya Send utapokea namba maalum kwa njia ya SMS kisha weka namba hizo kwenye kichumba maalum kwenye programu yako ya Twitter utapokea Backup Code hizo ni muhimu sana hifadhi code hizo kwani utakapo poteza simu au line zitakusaidia kuingia kwenye akaunti yako.

  • Jinsi ya kuzuia Akaunti ya Facebook Kuhackiwa (Kompyuta)

Ingia kwenye ukurasa wa facebook kisha login kwenye akaunti yako kisha bofya kamshale kalichopo upande wa kulia juu, baada ya hapo bofya kwenye Settings kisha bofya Securty and Login liyoko upande wa kushoto.

Baada ya hapo utaona sehemu iliyoandikwa Set up two-factor authentication bofya hapo kisha bofya edit kisha chagua aina moja ya ulinzi ambayo utapenda kuitumia, kwa sisi tutachangua ya Text Message (SMS) hivyo kila mara utakapo taka ku-login kwenye akaunti yako utapewa namba maalum ambazo unatakiwa kuziweka kwenye akaunti yako ili kuingia.

Kumbuka sehemu hii haitaweza kufanya kazi kama hujaweka namba yako ya simu hivyo kama hujaweka namba ya simu wakati unataka kuweka sehemu hii facebook itakutaka kuweka namba zako za simu ili kuwezesha sehemu hii.

Kama tayari umesha weka namba yako ya simu bofya Enable kisha bofya Continue bofya tena Continue na baada ya hapo utatumiwa code maalum ambazo unatakiwa kuweka kwenye kichumba maalum kisha utakuwa tayari umewezesha sehemu hiyo. Hapo kila mara utakapo taka kuingia kwenye akaunti yako utatumiwa code maalu za kuweka kwenye profile yako ili kuingia.

  • Jinsi ya kuzuia Akaunti ya Facebook Kuhackiwa (Simu)

Kwa upande wa simu ingia kwenye App yako ya facebook kisha bofya mistari mitatu iliyoko kwa pembeni upande wa kulia juu kisha shuka chini na chagua Account Settings baada ya hapo bofya Securty and Login kisha shuka chini mpaka ukute sehemu iliyoa andikwa Use two-factor authentication kisha hapa kama hujaweka namba kwenye akaunti yako facebook itakutaka kuweka namba.

Kama ulisha weka namba yako ya simu bofya tiki kwenye kichumba mbele ya maneno Two-factor authentication kisha utatakiwa kuhakiki akaunti yako kwa kuweka password kisha bofya Continue kisha utatumiwa namba ambazo utaweka kwenye kichumba maalum kwenye ukurasa huo kisha utakuwa tayari umewezesha ulinzi kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Sasa kila mara utakapo ingia kwenye ukurasa wako wa facebook unatakiwa kuingiza code maalum utakazo tumiwa na Facebook.

  • Jinsi ya Kuzuia Instagram Kuhackiwa (Simu Pekee)

Kabla ya kuanza ni vyema ujue kuwa kuweka namba yako ya simu ni kitu cha msingi sana kwenye mitandao ya kijamii hii itakusaidia kuweka ulinzi zaidi na ubora wa akaunti yako. Baada ya kusema hayo ingia kwenye programu yako ya Instagram kisha bofya vitufe vitatu vilivyoko juu upande wa kulia kisha utapelekwa kwenye Settings.

Shuka mpaka chini utaona sehemu iliyo andikwa Two-Factor Authentication bofya hapo kisha bofya kitufe kilichoko kulia kwenye maneno Require Security Code baada ya hapo bofya Turn On kisha utatumiwa namba ambazo utatakiwa kuziweka kwenye kichumba kinacho onekana kwenye ukurasa huo.

Mpaka hapo utakuwa umeweka ulinzi kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook pamoja na Instagram. Kwa maujanja na habari za teknolojia endelea kutembea Tanzania tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupata habari kwa haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use