Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuroot Simu Yoyote ya Android Bila Kompyuta (2020)

Unaweza kuroot simu za Tecno, Huawei, Samsung, LG na nyinginezo
Jinsi ya Kuroot Simu Yoyote ya Android Bila Kompyuta (2020) Jinsi ya Kuroot Simu Yoyote ya Android Bila Kompyuta (2020)

Karibuni Tanzania tech, leo kwenye maujanja tutaenda kujifunza jinsi ya kuroot simu yoyote ya smartphone bila kutumia kompyuta, njia hii huweza kufanya kazi kwenye simu nyingi za Android ambazo hazina toleo jipya la mfumo wa uendeshaji.

Njia hii mara nyingi uweza kufanya kazi kwenye simu zenye uwezo wa Android 2.1 hadi simu zenye Android 6.0 na baadhi ya simu zenye Android 7.0. Ili kuweza kuelewa zaidi njia hizi zime gawanyika kwenye makundi mawaili yaani kundi la simu za makampuni ya Samsung, LG, HTC na Motorola pamoja na kundi la simu za Huawei, Tecno pamoja na simu nyingine kama iTel na nyingine.

Advertisement

  • Kuroot simu ni nini na kuna faida gani ?

Kabla ya kuanza ni vyema ukajua kidogo kuhusu kuroot simu, kama umesikia neno hilo mara nyingi na hujui lina maana gani basi ningependa nikujuze kuwa kuroot simu ni kitendo cha kuondoa mipaka kwenye mfumo wa uendeshaji (Android System Files) na kuruhusu baadhi ya programu kwenye simu yako kuweza kufanya mambo ya ziada ambayo awali yalikuwa yamezuiwa na watengenezaji wa simu yako (simu janja).

  • Faida na hasara za kuroot simu

Kuna faida na hasara mbalimbali za kuroot simu yako na hii mara nyingi inategemena ni kitu gani unataka kufanya kwenye simu yako, moja kati ya faida za kuroot simu hizi hutokana na kama unataka kuinstall programu ambazo zinaweza kukupa uwezo wa kufanya vitu vya ziada kwenye simu yako. Hasara kubwa za kuroot simu ni kuharibu simu yako na hii maranyingi inatokea kama hatua za kuroot simu yako zimekosewa. Pia unaweza kupoteza Warranty ya simu yako hivyo ni vyema kuwa makini kabla ya kufanya hatua hizi.

Jinsi ya Kuroot simu za Samsung, LG, HTC na Motorola (kuwa makini hatuta husika ukiharibu simu yako)

Kwa kuanza hakikisha unatumia simu hizo hapa juu na hakikisha toleo lako la Android ni kuanzia Android 2.1 hadi toleo la Android 7.0, Vilevile hakikisha kuwa simu yako ina chaji angalau asilimia hamsini. Pia hakikisha simu yako ina internet kwani tutaenda kutumia programu ambayo ni lazima kudownload kwenye simu yako. Kama unayo mambo yote basi fuata hatua zifuatazo.

  1. Fungua kisakuzi cha simu yako kisha bofya hapa > Kingo Root
  2. Download na install App hiyo kwenye simu yako
  3. Fungua App hiyo kisha utaletewa ukurasa unao kuitaji kuwasha App hiyo kwenye sehemu ya Accessibility, bofya OK kisha shuka chini kidogo mpaka sehemu ya Kingo Optimization kisha bofya ON.
  4. Subiri kwa muda inaweza kuchukua muda kama wa dakika moja au zaidi inategemeana na simu yako,
  5. Baada ya hapo utona maneno Root succeeded hii ikiwa na maana umefanikiwa ku-root simu yako. (kama utona roote failed zima simu yako alafu washa kisha anza tena hatua hizi).

Jinsi ya kuroot simu za Huawei, Tecno na iTel (kuwa makini hatuta husika ukiaribu simu yako)

Njia za kuroot simu za tecno, Huawei na iTel ni tofauti na njia ya kuroot samsung, unaweza kujaribu kutumia programu ya Kingo Root kwenye simu hizi lakini kama programu hizi zitakataa basi unaweza kufuata hatua hizi zifuatazo.

  1. Download programu ya Framaroot hapa > Frama Root
  2. Install programu hiyo vizuri kwenye simu yako
  3. Washa programu ya Frama Root kisha chagua kati ya Superuser au SuperSU (unaweza kuchagua hii baada ya sehemu moja kushindwa) Kumbaka kuwa makini na simu yako.
  4. Kisha kwa chini yake chagua Boromir au option nyingine.
  5. Baada ya kuchagua sehemu hiyo utaona simu yako ikianza kuroot
  6. Baada ya hapo zima na washa simu yako, itakuwa tayari imekuwa rooted
  7. Kama hatua hizo zimekataa rudia hatua ya 3 kwa kuchagua option nyingine pia rudia hatua ya 4 kwa kuchagua option nyingine.
  8. Kujua zaidi kuhusu kuroot simu za Tecno soma HAPA

Mpaka hapo utakuwa umefanikisha kuweza kuroot simu yako ya Android bila kuwa na kompyuta, kumbuka njia hizi kwa namna moja ama nyingine zinaweza zisifanye kazi kwenye simu yako na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na sababu kubwa ya aina ya toleo la Android.

Kama una maswali au kuna mahali umekwama usiache ku-uliza hapo chini kwenye sehemu ya maoni nasi tutakuwa na furaha kujibu maswali yenu yote.

17 comments
  1. najaribu ku root sim yangu tecno cx air lakini frama root aikubali inaandika my phone seems vulnerable na haiendelei tena

  2. najaribu ku root sim yangu tecno cx air lakini frama root aikubali inaandika my phone seems vulnerable na haiendelei tena msaada tafadhali

  3. Xhida yangu nataka ku root simu yangu huawei kila nikipata maelezo yenu inagoma naomba unielekeze mbinu nyingine

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use