Tovuti za Kukusaidia Kufanya Mahesabu Magumu Kwa Urahisi

Sasa rahisisha mahesabu kwa kutumia tovuti hizi
Tovuti za kufanya hesabu Tovuti za kufanya hesabu

Wote tunajua kuwa kuna wakati hesabu zinasumbua kidogo kichwa, iwe wewe ni mwanafunzi au hata wewe ni mfanya biashara lazima kwa namna moja ama nyingine utakuwa unakutana na mahesabu.

Lakini leo hapa ninaenda kuzungumzia kitu cha tofauti kidogo, leo ninaenda kukuonyesha tovuti ambazo zinaweza kukusaidia sana hasa kwenye maisha ya mahesabu. Tunajua kuwa tunapo elekea ni kwenye ulimwengu wa teknolojia hivyo haitakiwi wewe kuendelea kuumiza kichwa wakati kompyuta au simu yako ya mkononi inaweza kukusaidia kufanya mahesabu yako ya kila siku.

 Basi bila kupoteza muda twende nikujuze kuhusu tovuti hizi, kumbuka unaweza kutumia tovuti hizi kwenye kifaa chochote iwe kwenye simu, kompyuta au hata tablet yako. Vilevile baadhi ya tovuti hizi zinayo programu maalum za simu (Application) hivyo kurahisisha sana kwa wanaotumia simu.

Advertisement

  • Omni Calculator

Omni Calculator ni moja kati ya tovuti yenye uwezo mkubwa sana wa kurahisisha maisha yako ya mahesabu ya kila siku. Tovuti hii ina calculator zaidi ya 379 ambazo zina uwezo wa kufanya mahesabu mbalimbali, iwe ni mahesabu ya biashara, afya, mahesabu ya kikemia, pamoja na mahesabu mengine mengi.

TEMBELEA TOVUTI YA OMNI CALCULATOR

  • Cymath

Cymath ni moja kati ya tovuti za siku nyingi sana, tovuti hii ni rahisi sana kutumia na inakusaidia kufanya mahesabu mbalimbali hasa yale ya darasani. Tovuti hii pia ina programu za Android na iOS na unaweza kupakua programu hizo kufanya mahesabu kwenye simu yako.

TEMBELEA TOVUTI YA CYMATH

  • Cymath – Math Problem Solver – Android
  • Cymath – Math Problem Solver – iOS
  • MathWay

Mathway ni tovuti nyingine yenye mfumo wa Calculator ambayo inaweza kukusaidia kufanya mahesabu kwa urahisi sana. Kwa wale wenzangu na mimi mliokuwa mnateseka na log (logarithm) basi hii ni calculator bora sana kwako mbali na uwezo wa kufanya hesabu za logarithm Mathway inaweza kukusaidia kufanya hesabu nyingi mbalimbali.

TEMBELEA TOVUTI YA MATHWAY

  • Symbolab

Symbolab ni aina nyingine ya calculator yenye nguvu na uwezo wa kufanya mahesabu magumu, Calculator hii inakupa uwezo wa kufanya mahesabu mbalimbali kama matrices pamoja na mehesabu mengine ya kutumia graph, calculator hii ina nguvu sana na ni nzuri kwaajili ya wanachuo na wanafunzi mbalimbali.

TEMBELEA TOVUTI YA SYMBOLAB

BONUS

Kuongezea hapo kwenye list hii hizi hapa chini ni programu za Android ambazo unaweza kutumia kufanya mahesabu mbalimbali, programu hizi ni rahisi kutumia na una weza kuinstall kwenye simu yako sasa.

  • MalMath: Step by step solver
  • Photomath
Photomath
Price: Free

Photmath ni programu ambayo inayoweza kufanya mahesabu kwa kupiga picha swali, yani unapiga picha swali kwa kutumia kamera ya simu yako ndani ya programu hiyo kisha programu hiyo inakupa majibu ya swali lako. Unaweza kujifunza zaidi HAPA.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use