Instagram Kuruhusu Hashtag na Kumtag Mtu Kwenye Bio

Sasa utaweza kuonyesha akaunti zako zingine au hashtag kupitia Bio
Instagram hashtag kwenye Bio Instagram hashtag kwenye Bio

Baada ya Instagram kusemekana kujiandaa kuja na sehemu mpya ya Focus, hivi leo mtandao huo umetangaza kuja na sehemu mpya itakayo kuruhusu kuweza kuweka hashtag pamoja na kuweka akaunti yako au ya mtu mwingine kwa kutag akaunti hiyo kupitia sehemu ya Bio.

Hapo hawali sehemu ya Bio au sehemu ya wasifu kwenye mtandao huo ilikuwa inaruhusu kuweka maandishi, pamoja na emoji na yote hayo ulikuwa unaruhusiwa kufanya kwa idadi ya maneno 150 pekee. Ingawa bado idadi ya maneno ni 150 lakini sasa uwezo wa kuweka hashtag na kuweka akaunti nyingine kwenye bio unaweza kutoa nafasi zaidi ya watu kueleza zaidi kuhusu akaunti zao.

Sehemu kwa sasa itakuruhusu kuweka hashtag na kutag akaunti nyingine lakini, endapo utaweka tag ya akaunti ya mtu kwenye sehemu yako ya Bio, basi yule ulie mtag atatumiwa ujumbe kutaka ajue kuwa ume mtag kwenye akaunti yako na instagram itampa huyo mtu uwezo wa kuzima tag hiyo kwenye ukurasa wako wa instagram kupitia sehemu ya Bio.

Advertisement

Kwa sasa sehemu hiyo iko kwenye akaunti zote za instagram, unaweza kujaribu sehemu hiyo kisha tupe maoni yako unaoneaje sehemu hiyo mpya itakusaidia kujieleza zaidi hasa kwenye sehemu ya Bio. Tuambie hapo chini kwenye sehemu ya maoni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use