Tovuti ya Kupakua Video za YouTube KeepVid Yasitishwa

Utoweza kupakua video bali utapata Takwimu kuhusu upakuaji Video
KeepVid KeepVid

Katika hali ya kushangaza tovuti maarufu ya kupakua video za Youtube KeepVid, imebadilishwa na sasa haitoruhusu kupakua video bali sasa utapata ushauri pamoja na takwimu za kupakua video kwenye mtandao wa Youtube.

Tovuti ya KeepVid awali ilikuwa ni moja kati ya tovuti maarufu za kupakua video za YouTube huku ikiwa ni tovuti ya 1,123 kwa umaarufu duniani kwa mujibu wa mtandano wa Alexa. Hata hivyo kampuni iliyokuwa inahusika na mtandao huo haijasema chochote kuhusu sababu za kubadilishwa kwa tovuti hiyo, bali kupitia msemaji wa kampuni hiyo ali wahakikishia watumiaji wa mtandao huo kuwa ni kweli huduma za tovuti hiyo zimesimamishwa na haitakuwa inafanya kazi kama awali.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC ambao ulifanya mahojiano na kiongozi wa mtandao huo ambaye alisema, “Upakuaji wa video utawezekana ikiwa zana za kupakua video na tovuti zenye video zitafikia makubaliano kuhusu upakuaji wa video,” kitu ambacho alisema ni kigumu.

Advertisement

Kwa sasa unaweza kupakua video kupitia ndani ya App za mtandao wa Youtube ambapo utaweza kuangalia video hizo lakini hutoweza kuzituma kwa mtu au kwenye kifaa chako kingine zaidi ya ndani ya app ya mtandao wa YouTube.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use