Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mark Zuckerberg Aomba Msamaha Zaidi Kupitia Magazeti

Atumia ukurasa mzima wa magazeti kuomba msamaha kwa watumiji wa FB
Mark Zuckerberg Facebook Cambridge Analytica Mark Zuckerberg Facebook Cambridge Analytica

Ni wazi kuwa sakata la Facebook na kampuni ya Cambridge Analytica ni moja kati ya taarifa kubwa sana za wiki hii na hata wiki iliyopita. Lakini pia ni wazi kuwa sakata hilo ni moja kati ya vitu vinavyo rudisha nyuma facebook kimafanikio kwa namna moja ama nyingine.

Kutokana na uzito wa swala hili, Mark Zuckerberg ambaye ndio mgunduzi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Facebook hivi karibuni alijitokeza rasmi kwenye mahojiano na kituo cha utangazaji cha CNN na kuomba msamaha kwa yale ambayo yalitokana na utumaji wa data za watumiaji wake ambao ulisemekana kufanywa na kampuni ya Cambridge Analytica.

Advertisement

Lakini kama haitoshi, siku ya jana Zuckerberg aliomba tena msamaha kwa kutumia kurasa nzima za magazeti ya The Observer, The Sunday Times, Mail on Sunday, Sunday Mirror, Sunday Express na Sunday Telegraph. Magazeti mengine ya marekani yalikuwa, The New York Times, The Washington Post, pamoja na The Wall Street Journal.

Barua hiyo ambayo ilichukua kurasa nzima ya magazeti hayo, ilikuwa ikiwataka wapenzi na watumiaji wa mtandao huo kuamini tena mtandao huo huku ikieleza hatua zilizochukuliwa na kampuni hiyo baada ya kujulikana kwa sakata hili.

Siku za karibuni Hisa za kampuni ya Facebook zinaonekana kushuka zaidi ikiwa pamoja na idadi ya watu wanaotumia matangazo ya Facebook kutangaza biashara zao kwa nchi za marekani na ulaya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use