Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Game Nzuri za Kucheza Mtu Zaidi ya Mmoja Kupitia Android

Game hizi zinafanana sana na Game kama PUBG na Fortnite
Game Nzuri za Kucheza Mtu Zaidi ya Mmoja Kupitia Android Game Nzuri za Kucheza Mtu Zaidi ya Mmoja Kupitia Android

Kama wewe ni mpenzi wa Game ni wazi unafahamu game ya PUBG, Game hii ni moja kati ya game nzuri sana na uzuri wake unatokana na uwezo wake wa kucheza mtu zaidi ya mmoja. Sasa mbali na game ya PUBG, zipo games nyingine nzuri sana kama PUBG ambazo unaweza kucheza na ndugu jamaa na marafiki moja kwa moja kupitia simu yako ya Android.

Kupitia makala hii ya leo nitaenda kuonyesha game hizo ambazo zinafanana sana na PUBG na ambazo unaweza kucheza na ndugu, jamaa na marafiki moja kwa moja kupitia simu yako ya Android. Kama wewe ni mpenzi wa game ya PUBG basi ni vyema kusoma makala hii hadi mwisho kwani nakuahidi lazima utafurahia game hizi nzuri, basi bila kupoteza muda wako zaidi twende tukangalie game hizi.

Advertisement

Cyber Hunter
Price: Free

Cyber Hunter ni game nzuri ambayo inafanana na PUBG, game hii inakupa uwezo wa kucheza game hiyo na ndugu na jamaa kwa urahisi sana. Ndani ya game hiyo kama ilivyo PUBG unatakiwa kupigana na wachezaji wengine hadi utakapo baki mwenyewe na hapo utakuwa umeshinda au umemaliza level fulani.

RULES OF SURVIVAL
Price: Free+

Game nyingine nzuri sana ya kujaribu kwenye simu yako ya Android ni Rules of Survival, Game hii ni nzuri na inafanana kabisa na PUBG, Game hii haina tofauti na game hiyo kwani inauwezo wa kuchezwa na watu zaidi ya wawili, unaweza kupakuwa game hii kupitia link hapo juu.

Creative Destruction
Price: Free+

Game nyingine ya kucheza na wenzako kwenye simu yako ya Android ni Game ya Creative Destruction, game hii ni tofauti kidogo na PUBG lakini inakuja na uwezo uleule wa kucheza mtu zaidi ya mmoja. Kwenye Game hii unatakiwa kuchukua roboti ambao wanabadilika kuwa kama magari na utapambana na roboti wengine kama hao hadi pale utakapo baki mwenye hapo ndipo utakuwa umeshinda Level moja kwenda nyingine.

Game nyingine nzuri ya kujaribu kwenye simu yako ya Android ni pamoja na Game ya Guns of Boom, Game hii ni nzuri sana na inafanana na PUBG kwa kiasi fulani. Kupitia game hii utaweza kucheza wewe na watu wengine wa nne na timu itakayobaki basi ndio mtakuwa mmeshinda.

Game nyingine ambayo ni nzuri sana na game ya Call of Duty, Game hii bado haijatoka ila unaweza kujisajili kupata game hii wakanza pale itakapo toka rasmi. Game hii inasemekana kuwa game hii itakuwa bora na inawezekana kupita hata game ya PUBG pamoja na Fortnite.

Na hizo ndio games ambazo nimekuandalia leo ambazo zinafanana sana na game ya PUBG, kama umependa game hizi unaweza kutuambia kwenye sehemu ya maoni hapo chini. Habari nyingine za teknolojia hakikihsa unatembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use