Kampuni ya Google Kusitisha Programu ya Allo Mwaka 2019

Baada ya kushindwa kufikia malengo Google yasitisha huduma za Google Allo
App ya Google Allo kusitishwa App ya Google Allo kusitishwa

Miaka miwili iliyopita kampuni ya Google iltangaza ujio wa app yake mpya kwaajili ya kuchat inayoitwa Google Allo, kuanzia kipindi hicho hadi sasa app hiyo imeshindwa kufanya vizuri na kufikia malengo ya kampuni hiyo ndio maana leo Google imetangaza rasmi kusitisha huduma za app hiyo ifikapo mwaka 2019.

Google Allo ni programu inayokupa uwezo wa kuchati na ndugu na jamaa kwa urahisi kupitia simu za Android na iOS. App hii haina tofauti sana na programu ya WhatsApp kwani inakupa nafasi ya kuweza kuchat, kutuma video na picha pamoja na kutumiana stika mbalimbali.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kutoka Google, App hiyo ya Google Allo inategemea kuzimwa kabisa hapo ifikapo mwezi March mwaka 2019. Google pia imeandika kuwa kwa kipindi chote kuanzia sasa watumiaji wa app hiyo watapewa nafasi ya kuweza kupakuwa data zao za muhimu ikiwa pamoja na kufuta kurasa zao kutoka kwenye app hiyo.

Advertisement

Google inategemea kuanzisha huduma mpya ya RCS ambayo inategemewa kuwa ni sehemu mpya itakayo kuwa badala ya sehemu ya SMS, sehemu hii itakupa uwezo wa kutuma picha, video kama inavyokuwa kwenye WhatsApp lakini hii ni kupitia sehemu yako ya kawaida ya SMS. Hata hivyo Huduma hii mpya ni lazima ifanyike kwa kutegemeana na kampuni zinazotoa huduma za simu, hivyo kwa hapa Tanzania itabidi kusubiri kidogo mpaka hapo kampuni za simu zitakapo kuwa na uwezo wa kufanya kazi na teknolojia hii.

Kwa sasa kampuni inayotoa huduma za simu ya nchini marekani Verizon, inasemekana imesha weza kuwa na teknolojia ya RCS na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali mtandaoni, siku ya leo kampuni hiyo inatarajia kuzindua huduma hiyo kwenye simu za Google Pixel 3.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use