Tetesi Kuhusu Programu ya Google Allo Kutoka Wiki Hii

Kwa wale wapenzi wa programu za kuchati mkae tayari kwani Google inaweza kuachia Programu yake ya Google Allo wiki hii
google-allo-kutoka-wiki-hii google-allo-kutoka-wiki-hii

Google Duo na Allo, ni programu zilizotangazwa na kampuni ya Google kwenye mkutano wake wa Google I/O uliofanyika mapema mwaka huu huko nchini marekani, lakini mpaka sasa programu moja tu ndio iliyo fanikiwa kutoka ambayo ni programu ya Google Duo. Programu hiyo ambayo kwa sasa inafanya vizuri kwa kuwa na downloads zaidi ya milioni 10,000,000 imefanya mzunguko wa programu za kuchat duniani kuongezeka.

Hivi karibuni mzunguko huo unatarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na tetesi zinazosema kuwa huenda Google ikaachia programu yake ya Google Allo, tetesi hizo zikiwa zimandikwa kwenye tovuti ya teknolojia ya Android Police ziliongeza kuwa programu hiyo inaweza kuja mapema wiki hii na kufuatiwa na toleo jipya (update) la programu ya Google Duo.

Kama bado ujaji sajili kupokea programu hiyo unaweza kufanya hivyo kwa kubofya hapo chini kisha jisajili moja kwa moja ili kuwa wa-kwanza kupata programu hiyo mpya ya kuchat mara tu inapoachiwa na kampuni maarufu ya Google.

Advertisement

TAARIFA MPYA LEO 21-09-2016
Hatimaye programu hiyo mpya ya kuchat imetoka leo rasmi na tayari imesha downloadiwa na watu mbalimbali dunia, muda si mrefu kuanzia leo Tanzania pia tutaweza kudownload programu hii moja kwa moja kwenye simu za android bila kusahau pia iOS. Mpaka hapo itakapo tufikia Tanzania tech tutakua tukiwa Habarisha kuhusu programu hii mpya kutoka kampuni ya Google.

iOS

Google Allo
Price: Free

Android

Google Allo
Price: Free

Pia unaweza kupata taarifa za programu hii pindi tu itakapo toka kupitia blog ya tanzania tech, jinsi ya kufanya ni rahisi sana cha msingi endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use