Sasa Link za Video Kuonyesha Video Ndani ya WhatsApp

Watumiaji wa Android sasa kuangalia link za video ndani ya WhatsApp
Link za video WhatsApp Link za video WhatsApp

Kama wewe ni mmoja wa wafuatiliaji wa maswala ya teknolojia basi lazima utakuwa unajua kuwa hivi karibuni WhatsApp ilikuwa ikifanya majaribio ya kufanya link za video unazotumiwa kupitia WhatsApp ziweze kufungua video ndani ya WhatsApp na sio hadi kwenda kwenye website husika.

Hatimaye majaribio hayo siku za karibuni yamekamilika na sasa unaweza kuangalia video ndani ya WhatsApp. Hapo awali pale mtu atakapo kutumia link ya video kwa mfano YouTube basi ni lazima uangalie video hiyo kupitia mtandao wa YouTube pale unapo bofya link hiyo.

Lakini sasa mambo ni tofauti kidogo kwani pale mtu atakapo kutumia Link ya video kwa mfano YouTube, utaweza kuangalia video husika ndani ya App ya WhatsApp bila kuingia kwenye app ya YouTube. Pale unapo tumiwa link ya video bofya kitufe cha Play na moja kwa moja video itaanza kucheza hapo hapo.

Advertisement

Unaweza kuangalia video za mitandao kama Facebook, Instagram, YouTube, Vimeo, Dailymotion na tovuti nyingine nyingi zenye kuonyesha video. Kwa sasa sehemu hii inapatikana kwenye app ya WhatsApp ya Android. Kwa watumiaji wa iOS sehemu hii tayari ilisha wezeshwa mapema miezi kadhaa iliyopita, kama wewe unatumia android na bado hujapata uwezo wa kucheza video ndani ya WhatsApp unaweza ku-update app ya WhatsApp kupitia Play store ili kupata sehemu hiyo.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use