Google Kuja na CHAT Sehemu Mpya ya Android Badala ya SMS

Sasa Sehemu hiyo itakuwezesha kutuma picha pamoja na sauti
Google Kuja na CHAT Sehemu Mpya ya Android Badala ya SMS Google Kuja na CHAT Sehemu Mpya ya Android Badala ya SMS

Miaka miwili iliyopita hapa Tanzania Tech tulishawahi kuongelea kuhusu Google kuja na sehemu mpya ambayo itakuwa badala ya SMS kwenye simu za Android, kwenye makala hiyo tulisema mfumo huo utakao tumika unaitwa RCS au Rich Communication Services. Sasa toka mwaka huo 2016 hadi kufikia sasa, kampuni ya Google imetangaza rasmi kuanza kutumia mfumo huo kwenye simu za Android na utakuwa badala ya sehemu ya SMS, hivyo sasa itakuwa ni CHAT na sio SMS.

Kitu cha kuzingatia hapa ni kwamba, ni lazima mtandao wako wa simu uweze kuwa na uwezo wa mfumo huo wa RCS au Rich Communication Services. Mbali na hayo kama wewe na unae mtumia meseji wote mitandao yenu ya simu inayo uwezo wa mfumo huo wa RCS, basi yeyote kati yenu hato chajiwa kwa SMS, bali mtakuwa mna chajiwa kwa bando au Data mnayo tumia. Kingine kizuri kuhusu mfumo huu mpya ni kuwa kama mmoja wenu au wote mitandao yenu ya simu haina uwezo wa RCS, basi mtaendelea kutumia sehemu hiyo mpya ya CHAT kama ilivyo SMS kwa sasa na mtakuwa mnakatwa garama za kawaida za SMS.

Kwa kifupi ni kuwa, mfumo huu utakuwa ufanya kazi sawasawa na ilivyo iMessage ya kwenye mfumo wa iPhone, utakuwa na uwezo wa kutuma picha, sauti au hata kuchati kwa kutumia ma-group mbalimbali lakini utofauti utakuwa kwenye ulinzi kwani, sehemu hiyo ya CHAT kupitia mfumo wa RCS yenyewe inafanya kazi sawasawa na mfumo wa kawaida wa SMS, hivyo ni lazima meseji zako zihifadhiwe kwenye Server ya mtandao wako wa simu bila kuwa encrypted ndipo zitumwe kwa muhusika, tofauti na mfumo wa iMessage ambapo meseji hizo zinakuwa encrypted ndipo zitumwe.

Advertisement

Tofauti na hapo ni kuwa, Google imeleta sehemu hii ili kuboresha SMS hivyo, hakuna kitu chochote kitakacho ondolewa kwenye sehemu yako ya kawaida ya SMS, bali sehemu hiyo inaongezewa uwezo wa kutumia mtandao hivyo utakuwa na uwezo wa zaidi wa kutuma maandishi, picha na sauti kupitia sehemu ya kawaida ya Meseji ikiwa pamoja na kutumia sehemu yako ya Meseji ya Android kupitia kompyuta yako bila kutumia programu nyingine yoyote na hiyo yote ikiwa ni kwa gharama za mtandao au data na sio gharama za kawaida za SMS au MMS.

Google tayari imesha tangaza kushirikiana na kampuni mbalimbali za simu ili kuweza kuleta sehemu hiyo kwenye simu nyingi za Android pamoja na mitandao ya simu, Kampuni kama Samsung, LG, Microsoft na nyingine nyingi zimesha kubaliana na Google hivyo tegemea kuona sehemu hii kwenye simu nyingi za Android siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use