Samsung Kulipa $10 Kwa kila Aliyenunua Simu ya Galaxy S4

Kama uliwahi kuwa mmiliki wa Galaxy S4 basi jiandae kupata $10
Samsung Kulipa $10 Kwa kila Aliyenunua Simu ya Galaxy S4 Samsung Kulipa $10 Kwa kila Aliyenunua Simu ya Galaxy S4

Samsung Galaxy S4 ni moja kati ya simu ambazo nadhani zilifanikiwa kuuza nakala nyingi sana kwa kipindi cha mwaka 2013, lakini pia kipindi hicho watu wengi sana walikuwa hawajali sana uwezo wa simu pengine hii ndio sababu ya watu wengi kutokujua baadhi ya matatizo ya simu hizo.

Sasa hapo jana habari mpya kutoka tovuti ya Theregister zidai kuwa, kampuni ya Samsung inatarajia kuwalipa wamiliki halali wa Galaxy S4 kiasi cha shilingi za kitanzania TZS 23,000 kila mmoja ambayo ni sawa na dollar $10 za marekani.

Samsung Kulipa $10 Kwa kila Aliyenunua Simu ya Galaxy S4

Advertisement

Hatua hiyo inakuja baada ya kampuni hiyo kushindwa kesi iliyokuwa inaendelea kutokea mwaka 2013, kesi ilikuwa inakabili kampuni ya samsung baada ya kugundulika kutumia programu maalum ambayo ilikuwa ikifanya simu hizo zionekana zina uwezo zaidi ingawa zilizilikuwa hazina uwezo huo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Android Police, Samsung ilikuwa inatumia programu maalum kuongeza uwezo wa simu hiyo pale inapo fanyiwa majaribio kupitia Benchmarks, ripoti hiyo inadai kuwa kwa kawaida simu ya Galaxy S4 ilikuwa inakuja na GPU frequency yenye uwezo wa hadi MHz 480, lakini mara baada ya simu hii kufanyiwa marajibio kupitia Benchmarks ilionekana kubadilika na kuwa na GPU frequency ya MHz 532 ambayo ni sawa na ongezeko la GPU frequency kwa asilimia 11%.

Samsung Kulipa $10 Kwa kila Aliyenunua Simu ya Galaxy S4

Hata hivyo inasemekana kuwa Samsung ilikuwa inatumia moja ya programu kuweza kuongeza uwezo kwenye baadhi ya programu za simu hiyo, ili simu hiyo iweze kuonekana kuwa na uwezo mkubwa ijapokuwa kampuni hiyo inajua kabisa kuwa huo ni udanganyifu. Kama unataka kujua zaidi kuhusu kesi nzima jinsi ilivyokuwa unaweza kusoma zaidi hapa.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamewahi kumiliki simu hiyo kwa kununua kabisa kutoka dukani, basi usiwe na haraka kwani hadi sasa bado haijajulikana ni utaratibu gani Samsung itatumia kuweza kugawa fedha hizo kwa wamiliki wa simu hizo au watu ambao wamewahi kununua simu hizo kuanzia mwaka 2013 muda ambao ndio simu hizo zilizinduliwa rasmi.

Ili kujua hatua ambazo unatakiwa kufuata ili kulipwa pesa hizo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza pindi utaratibu huo utakapo tangazwa rasmi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use