Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Facebook Yaja na App ya Facebook Messenger Kwaajili ya Watoto

Sasa watoto wataweza kuchati kwa uhuru kwa ruhusa ya wazazi
Facebook Messenger Kids Facebook Messenger Kids

Ulimwengu wa teknolojia na mawasiliano unaonekana kukuwa kila siku kiasi kwamba imekuwa na muhimu hata kwa watoto wetu. Facebook kwa kuliona hilo sasa imekuja na programu mpya ya Facebook Messnger kwaajili ya watoto.

Advertisement

Tofauti na programu ya kawaida ya Facebook Messenge, App hii mpya kwaajili ya watoto inampa mzazi nafasi ya kuweza kuchagua ni watu gani ambao angependekeza mwanae achati nao. Mtoto atakapo hitaji tumia app hiyo mzazi pekee ndio ataweza ku-install programu hiyo kwenye kifaa cha mtoto.

Mbali na hayo programu hiyo haina mambo ya manunuzi hivyo kuweza kumzuia mtoto kutokutumia pesa za wazazi kununua vitu mbalimbali, programu hiyo pia itawawezesha watoto kuweza kutumiana video na picha mbalimbali zenye sticker zenye maadili.

Kwa sasa App hiyo inapatikana kupitia vifaa vya Apple vya iPhone, iPad, na iPod Touch, lakini pia programu hii haipatikani kila nchi hivyo kama unaona bado programu hiyo haikubali kwenye kifaa chako usijali kwani inawezekana programu hiyo haija tolewa rasmi nchini kwako.

‎Messenger Kids
Price: Free

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use