Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Kupitia app hizi utaweza kuangalia movie na TV Series moja kwa moja
Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuwatakiwa heri ya mapema ya Christmas na mwaka mpya kwenu nyote, hakika Mwenyezi Mungu ametupendelea wote na leo tupo pamoja mwezi wa mwisho wa mwaka na kwa mapenzi yake tutasherekea mwisho wa mwaka. Ni wazi kuwa tuna wajibu wa kumshukuru Mungu na kuendelea kuomba kila siku.

Kwa kuwa najua kipindi hiki watu wengi wanakuwa likizo, basi nimeona niwaletee makala hii fupi ambayo utaweza kujua apps nzuri ambazo unaweza kutumia ku-stream movie bure bila kulipia. Kupitia apps hizi pia utaweza ku-download movie hizi na kuangalia bila Internet ndani ya apps hizo.

Basi bila kuendelea kupoteza muda zaidi moja kwa moja twende tukangalia apps hizi, kumbuka apps hizi nyingi hazipo kwenye soko la Play Store hivyo kama unataka kupakua app yoyote unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe chini ya maelezo ya apps husika.

Advertisement

Plex Stream Movies

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Plex ni moja kati ya app bora sana ya kustream movie pamoja na series bure kabisa bila kulipia, app hii inafanyakazi kwenye TV pamoja na kwenye simu yoyote yenye mfumo wa Android. Uzuri wa app hii utaweza kupakua filamu au series mpya kwa haraka kabisa kupitia vyanzo mbalimbali. Unaweza kujaribu app hii kwa kupakua hapo chini kisha niambie kupitia maoni umeonaje app hii.

Download App Hapa

VIU Premium

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Kama wewe ni mpenzi wa movie na tamthilia mbalimbali za kutoka india, Nigeria, Kenya, Korea, Ghana, Pakistani na nchi nyingine basi app hii itakufaa sana. App hii inakuja na filamu nyingi pamoja na tamthilia ambazo unaweza kuangalia ndani ya app hii moja kwa moja au kwa kudownload moja kwa moja kupitia kwenye app hiyo, app hii pia inakuja na movie za Kiswahili.

Download App Hapa

ZiniTevi

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

ZiniTevi ni app nyingine nzuri ambayo unaweza kutumia ku-stream movie kupitia simu, smartTV kupitia Laptop na hata vifaa vingine vya kidigital. App hii ni moja kati ya app nzuri sana ya kugundua movie mpya na inakuja na njia bora sana ya kutambua movie mpya na ku-stream bure bila kulipia. Pia unaweza kudownload na kuangalia movie hizo ndani ya app hii.

Download App Hapa

Tubi Pro

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

Tubi pro ni app nyingine ambayo itakusaidia ku-stream movie kwa urahisi kupitia simu yako, app hii nayo inakuja na mchanganyiko wa filamu pamoja na tamthilia ambazo unaweza kuangalia au ku-stream moja kwa moja kwenye simu yako ya Android. Unaweza kuangalia movie bila kulipia.

Download App Hapa

HD Movies

Apps Nzuri za Android za Ku-stream Movie Bure Bila Kulipia

App ya mwisho kwenye list hii ni HD Movies app hii itakupa uwezo wa kuangalia movies zote kwa urahisi na kupitia simu yako ya Android. App hii haina tofauti sana na app nyingine kwenye list hii kwani nayo utaweza ku-stream movie ikiwa pamoja na kuhifadhi movie hizo ndani ya app hii na utaweza kuangalia bila kutumia internet.

Download App Hapa

Na hizo ndio app ambazo unaweza kutumia ku-stream movie moja kwa moja kwenye simu yako siku ya leo, kama utakuwa unataka apps zaidi unaweza kusoma hapa kujua apps nyingine za kudownload movie kwa urahisi kupitia simu yako hapa.

2 comments
  1. naomba msaada jinsi ya kurusha sms nilizofuta kwenye simu ndogo aina ya itel,?
    sms nilizofuta kwenye facebook kama ina wezekana .yabule bila kulipia zitumike mb?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use