Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

App hizi zitakusaidia kutumia simu ya Android iliyopo rooted kwa urahisi zaidi
Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao tayari umefanikiwa kuroot simu yako ya Android basi makala hii ni kwa ajili yako, kama kwa namna yoyote unataka kujifunza kuroot simu yako basi unaweza kusoma makala hii kama unataka kuroot simu ya TECNO, au hapa kama unataka kuroot simu ya Samsung. Kumbukua kuroot simu yako kuna madhara hivyo ni vyema kujua nini unachokifanya.

Sasa kama tayari umesha fanikiwa kuroot simu yako basi endelea moja kwa moja kwenye makala hii ambayo leo tutakuwa tukiangalia apps nzuri kwa ajili ya simu za Android ambazo zipo rooted. Baadhi ya apps hizi unaweza kutumia kwenye simu ambazo hazipo rooted, hivyo hata kama wewe huja root simu yako basi unaweza pia kusoma makala hii.

Advertisement

App2SD Pro

App2SD Pro ni app nzuri sana kwa watu wenye simu zenye uwezo mdogo wa ROM au ukubwa wa ndani, kama kwa namna yoyote unataka kuamisha apps kutoka kwenye ukubwa wa ndani kwenda kwenye memory card basi hii ni app nzuri sana kwa ajili yako. Uzuri wa app hii ni kuwa unaweza kuamisha apps zote kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye memory card, wote tunajua simu iliyojaa vitu vingi ina mtindo wa kuwa slow hivyo app hii itakusaidia sana kufanya simu yako kufanya kazi kwa urahisi na haraka.

Download App Hapa

Greenify

Greenify
Price: Free

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao simu yako ina tatizo la kuisha chaji mara kwa mara basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii inauwezo wa kipekee wa kutunza battery kwenye simu yako kwa kuzuia baadhi ya app kufanya kazi nyuma ya pazia, App kama Facebook, Instagram na nyingine zina mtindo wa kutumia data kwenye simu yako bila hata wewe kutumia app hizo. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuangalia app zinazotumia data zaidi kwenye simu yako.

Download App Hapa

Root Booster

Root Booster
Price: Free

Kama unataka kuongeza uwezo wa simu yako kwa haraka basi app hii ya Root booster ni app nzuri sana kwako wewe mwenye simu iliyopo rooted. App hii itakupa uwezo wa kuongeza RAM, Speed ya simu yako pamoja na uwezo wa kufanya simu yako idumu na chaji zaidi. App hii inaweza kufanya kazi kwa watu wenye simu zilizopo rooted na hata zile ambazo hazipo rooted.

Download App Hapa

DiskDigger Photo Recovery

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamewahi kupoteza picha kwa kufuta bahati mbaya na unayo simu ya Android iliyopo rooted basi habari njema kwako. Kupitia app ya Disk Digger unaweza kurudisha picha zilizo futika au kufutwa kwenye simu yako moja kwa moja, app hii inauwezo wa kurudisha picha zilizofutwa kwa urahisi na inaweza kufanya kazi kwenye simu ambazo pia hazipo rooted, lakini inafanya kazi zaidi kama simu yako ipo rooted.

Download App Hapa

System App Remover (Root needed)

System app remover
Price: Free

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanasumbuliwa na app ambazo zinakuja na simu basi app hii itakusaidia sana, App hii inauwezo mkubwa wa kuondoa apps mbalimbali ambazo zinakuja na simu ambazo huwezi kuziondoa kwenye simu yako ya Android.

Download App Hapa

Titanium Backup ★ root needed

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kufanya backup kwenye simu yako ya Android iliyopo rooted basi app hii ni muhimu sana kwako. App hii inauwezo mkubwa wa kubackup kila kitu kwenye simu yako ikiwa pamoja na apps zote unazo tumia pamoja na Call Log, SMS, Call Log na kila programu iliyopo kwenye simu yako ya Android.

Download App Hapa

Solid Explorer File Manager

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kuangalia au kubadilisha yote yaliyomo kwenye simu yako ya Android basi app hii ya Solid Explorer ni app nzuri sana kwako. App hii inakupa uwezo wa kuingia kwenye file za simu yako ikiwa pamoja na uwezo wa kubadilisha au kufuta file hizo kwa haraka kama simu yako ipo rooted. App hii ni vizuri kutumiwa na mtu anayejua anachokifanya kwani unaweza kuharibu simu yako bila kujua.

Download App Hapa

Wps Wpa Tester

WIFI WPS WPA TESTER
Price: Free

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kupata password ya WiFi yoyote unayotaka kutumia basi unaweza kutumia app hii. Unaweza kufuata hatua kwa hatua jinsi ya kutumia app hii kupitia hapa. App hii inaweza kufanya kazi kwenye simu yoyote ya Android lakini inafanya kazi vizuri kwenye simu ya Android iliyopo rooted.

Download App Hapa

Na hizo ndio baadhi tu ya Android app ambazo ni nzuri kwenye simu yako ya Android iliyopo rooted. Kama unajua app nyingine nzuri zaidi unaweza kuchangia kwa kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kujua app nyingine nzuri kwa ajili ya simu yako ya Android unaweza kusoma makala nyingine hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use