Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram

Zifahamu hizi hapa app nzuri za kukusaidia kutumia Instagram kwa urahisi
Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram

Instagram ni mtandao maarufu sana kwa sasa, kwa mujibu wa tovuti ya oberlo, hadi mwezi wa tatu mwaka 2022 Instagram Inatumiwa na zaidi ya watu Bilioni 1.3 kila mwezi, ikiwa ni mtandao wa pili kutumiwa na watu wengi zaidi duniani baada ya mtandao wa Facebook.

Sababu hii na nyingine nyingi ndio zinasababisha leo tukuletee makala hii ya Apps nzuri za kuweza kusaidia kurahisha matumizi ya mtandao wa Instagram.

Advertisement

Kumbuka Apps hizi nyingi zinapatikana kwenye soko la Play Store hivyo unaweza kudownload app hizo moja kwa moja kupitia soko la Play Store kwa kubonyeza link iliyopo chini ya jina la Apps husika, basi bila kupoteza muda zaidi twende tukangalie app hizi.

Unfollow for Instagram

Unfollow for Instagram - Non f
Price: To be announced

App hii ya Unfollow ni app nzuri sana kwa sababu inakupa urahisi wa kufollow watu kwa urahisi na pia ku-unfollow watu kwa haraka, app hii inaweza kusaidia sana kama wewe unataka kupunguza watu kwenye akaunti yako hasa wale ambao hawakufuati (Follow) lakini wewe unawafuata.

Download Hapa

Profile Photo Downloader for instagram

Kama kwa namna yoyote ungependa kuangalia au kudownload picha ya Profile ya mtu yoyote kupitia Instagram basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii itakupa uwezo wa kupakua Profile Picture au picha ya wasifu kwenye akaunti ya mtu yoyote ya Instagram.

Download Hapa

Repost for Instagram

Kama unahitaji kudownload picha ya mtu yoyote au unataka kurepost picha ya mtu kwenye akaunti yako ya Instagram basi app hii ni nzuri sana kwako, App hii itakupa uwezo wa ku-repost pamoja na ku-download picha yoyote kwa haraka kabisa.

Download Hapa

Tagify

Hashtag ni moja kati ya kitu muhimu sana ambacho kitakusaidia kufikia watu wengi sana kwenye akaunti ya Instagram, kama wewe unayo akaunti ambayo ungependa watu waijue kwa haraka basi hakikisha unatumia hashtags kwenye kila post yako. App hii ya Tagify itakusaidia kuchagua hashtag kulingana na picha unayotaka kupost.

Download Hapa

Apphi

Apphi ni app nyingine nzuri sana kwa ajili ya Instagram, App hii itakusaidia kuandaa post na kuziweka zijipost zenyewe baadae, kupitia app hii unaweza kuweka hata post za wiki nzima na zitaweza kujipost zenyewe kila siku.

Download Hapa

Unfold

Kama wewe ni mpenzi wa Instagram hasa sehemu ya Stories basi app hii itakusaidia sana, App hii itakusaidia kuweza kutengeneza picha au video nzuri ambazo unaweza kuweka kwenye akaunti yako kupitia sehemu ya Stories.

Download Hapa

Canva

Canva ni moja ya app ambayo tumzungumzia sana hapa Tanzania Tech, hii ni kwa sababu app hii ni nzuri sana na itakupa wepesi sana hasa kwenye kutengeneza post zako kwenye akaunti yako ya Instagram. Mbali na Instagram pia utaweza kutengeneza picha au vitu vingine mbalimbali kwa urahisi.

Download Hapa

Video Editor & Video Maker – InShot

Inshot ni moja ya app maarufu sana na bora sana kwa watumiaji wa Instagram, app hii inakupa uwezo wa kufitisha picha pamoja na video na kufanya ziwe na muonekano mzuri kupitia akaunti yako ya Instagram, kama mpaka sasa huna appa hii ni wakati wako kudownload sasa.

Download Hapa

Na hizo ndio baadhi tu ya apps ambazo unaweza kuzitumia na kurahisha matumizi yako ya mtandao wa Instagram, kumbuka unaweza kujifunza maujanja zaidi ya kurahisha kutumia akaunti ya Instagram kwa kusoma hapa. Kwa app nyingine nzuri unaweza kusoma kipengele cha Programu hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use