Hizi Hapa Apps Nzuri za Android Kwaajili ya Wanafunzi

Hizi hapa app bora kwako wewe mwanafunzi
App nzuri kwaajili ya wanafunzi App nzuri kwaajili ya wanafunzi

Ni wazi kuwa Android ni moja kati ya mfumo unaotumiwa na watu wengi zaidi, sababu hii na nyingine nyingi ndio maana leo nimeamua kuleta list hii ya app nzuri za Android kwa ajili ya wanafunzi. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie App hizi.

Exam Countdown Lite
Price: Free

Exam Countdown ni app nzuri ambayo itakusaidia kukupa kumbukumbu ya tarehe za mtihani pamoja na test mbalimbali, App ni nzuri sana kwa wale wanao weka ratiba ya kusoma kwani app hii itakuwa inakupa taarifa siku ngapi zimebakia hadi kufikia tarehe ya mtihani. Unaweza kudownload app hiyo kwa kutumia link hapo juu.

Download App Hapa

Advertisement

Kama wewe ni mwanafunzi na umekuwa mgumu kuamka hata pale alarm inapolia basi app hii ya Alarmy ni kwa ajili yako. App hii nakuja na njia ya kipekee ya kutoa kukuamsha kwani alarm hii inapo anza kulia hutoweza kuizima mpaka utoe jibu la hesabu inayokuja juu ya kioo cha simu yako. Mpaka utakapo maliaza kupata jibu la swali hilo bila shaka utakuwa umeamka kabisa.

Download App Hapa

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda kujua maana ya maneno mbalimbali ya kingereza basi app hii ya Oxford Dictionary ni nzuri sana kwako. App hii inakupa uwezo wa kujua maana ya maneno magumu ya kiingereza ikiwa pamoja na jinsi ya kuyatumia maneno hayo kwenye sentensi mbalimbali, pia app hii itakuwa inakupa neno la siku na maana yake.

Download App Hapa

Tukiwa tunaongelea dictaniary ni lazima kuongelea app hii ya English Swahili Dictionary, app hii itakuapa tafsiri ya kiswahili ya maneno mbalimbali ya kiingereza ikiwa pamoja na jinsi ya kutumia maneno hayo kwenye sentensi bila kusahau jinsi ya kuyatamka.

Download App Hapa

Socratic
Price: Free

Kama kuna swali la hesabu linalo kusumbua basi app hii ya Socratic ni msaada kwako wewe mwanafunzi, app hii inakupa uwezo wa kupiga picha swali na app hii itaweza kukupa jibu ya swali hilo moja kwa moja. Uzuri wa app hii ni ya bure kwa asilimia 100 hivyo huna haja ya kulipia pesa yoyote. Vilevile app hii itaweza kuonyesha njia za kuweza kupata jibu la swali ulilo uliza.

Download App Hapa

Kama unataka kubadilisha assignment uliyopewa kutoka kwenye karatasi na kuja kwenye PDF basi app hii ya Office lensi ni nzuri sana kwako. App hii itakusaidia kuweza kubadilisha picha za kawaida kuwa kwenye mfumo wa PDF.

Download App Hapa

All Formulas
Price: Free

Kama kwa muda mrefu umekuwa ukipata shida ya kanuni (Formula) kwenye masomo ya hesabu, physics na chemistry basi app ya All Formulas ni app nzuri sana kwako. App hii itakupa kanuni mbalimbali zinazotumika kwenye masomo mbalimbali ya Hesabu, Physics pamoja na Chemistry.

Download App Hapa

Na hizo ndio apps nzuri ambazo unaweza kuzitumia kama wewe ni mwanafunzi, Kwa wanafunzi kwa leo tunaishia hapa, ila Kama ungependa kujua jinsi ya kubadilisha rangi ya Navifation bar kwenye simu yako ya Android basi soma hapa. Kujua zaidi kuhusu habari za teknolojia na app nyingine nzuri endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

4 comments
  1. Habari, naomba kujua app ya Android inayoweza kutafsiri pdf, documents katika lugha zote ikiwemo kiswahili

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use