Hatimaye Kampuni za Simu za Tigo na Zantel Zaungana Rasmi

Sasa wateja wa Zantel watapata huduma bora za mtandao wa Tigo
Hatimaye Kampuni za Simu za Tigo na Zantel Zaungana Rasmi Hatimaye Kampuni za Simu za Tigo na Zantel Zaungana Rasmi

Miezi 10 iliyopita kulikuwa na ripoti kuhusu kampuni ya Tigo kumiliki kampuni ya Simu ya Zantel, Hatimaye hivi leo Kampuni ya mawasiliano ya MIC Tanzania PLC au Tigo, imetangaza rasmi kuungana na kampuni hiyo ya Zanzibar Telecom PLC au Zantel baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria na kiumiliki.

Kwa mujibu wa tovuti ya mwananchi, Taarifa iliyotolewa na Tigo inasema baada ya kupata vibali kutoka mamlaka zinazo husika, pamoja na mchakato wa kuhamisha hisa za kampuni ya Zantel kwenda Tigo kukamilika sasa kampuni hizo zitaungana katika shughuli zake za utendaji Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Hatimaye Kampuni za Simu za Tigo na Zantel Zaungana Rasmi

Advertisement

Akizungumza kuhusu muungano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari alisema hatua hiyo ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza kuhusu muungano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari alisema hatua hiyo ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa ujumla kwani kutajenga huduma jumuishi kwa watanzania wote siku za usoni kwani wateja wote wa Tigo na Zantel wataweza kufurahia huduma bora kutoka kwenye soko imara litakalosaidia kuchochea ubunifu kwenye sekta ya mawasiliano.

Hata hivyo inasemekana kuwa, zoezi la kuunganisha taratibu za kiutendaji wa makampuni hayo mawili zinatazamiwa kuanza hivi punde na wateja wote wa Tigo pamoja na Zantel wataendelea kupata huduma bila usumbufu wowote kutoka mtandao husika kwani namba na laini za wateja hazitabadilika.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use