Jinsi ya Kurekodi Simu Unazopiga na Kupigiwa (Android)

Njia rahisi ya kurekodi sauti ya mtu unayempigia au anayekupigia simu
Jinsi ya Kurekodi Simu Unazopiga na Kupigiwa (Android) Jinsi ya Kurekodi Simu Unazopiga na Kupigiwa (Android)

Kuna wakati unahitaji kurekodi sauti ya mtu anaye kupigia simu au unaepigia simu, hii inatokana na sababu mbalimbali za kimaisha ambazo pengine hatuna haja ya kuzitaja hapa. Kupitia makala hii ntaenda kuonyesha njia rahisi ambazo unaweza kutumia kurekodi sauti ya mtu unayeongea nae kwenye simu yako kwa haraka.

Kabla ya kuanza ni vyema ufahamu kuwa kurekodi maongezi ya mtu bila yeye kujua inaweza kuwa ni kosa la jinai hivyo ni vyema kuwa muangalifu sana unapofanya hivyo na pia ni muhimu kumjulisha mtu unaye ongea nae kama unarekodi maongezi yenu.

Hatua ya kwanza unatakiwa kupakua app inaitwa Call recorder, app hiyo inapatikana kwenye soko la Play Store pia unaweza kupakua app hiyo kupitia link hapo chini.

Advertisement

Call recorder
Price: To be announced

Baada ya kupakua na ku-install vizuri app hii kwenye simu yako sasa fungua app hiyo kisha ruhusu app hii kwenye simu yako kisha endelea kwenye hatua ya pili ambayo ni kupiga au kupigiwa simu. App hii itaweza kurekodi simu yako bila hata wewe kufanya kitu kingine chochote… rahisi ehh..

Kama kuna mahali utakuwa umekwama basi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi hakiksha unatembelea ukurasa wa maujanja kupitia hapa au unaweza kujifunza jinsi ya kusoma meseji za mtu bila yeye kujua kupitia makala hii hapa.

1 comments
  1. Mm simu yangu haina call record ni a20 ss nifanyaje?ukiweka app ya call record inashisndwa kurekodi inarekodi jinsi mm ninavyoongea tu yule ninaeongea nae haimrekodi.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use