Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Ziadi ya kutumia mitandao ya kijamii simu yako inaweza kukuokoa..
Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Ukweli ni kwamba simu za smartphone zimekuwa ni msaada mkubwa kwenye maisha yetu ya kila siku, huwenda unaichukulia poa sana simu yako kwa sababu umesha zoea kuwa nayo kila siku ila pengine umuhimu wa simu hizi huja pale unapokuwa huna simu hiyo.

Natumaini hadi sasa unayo simu yako kwani leo nitaenda kukwambia njia ambazo simu janja yako inaweza kusaidia kukuondoa wewe au watu wako wa karibu kwenye hali ya hatari. Kumbuka baadhi ya njia hizi zinafanya kazi kwenye simu zote za Android na iOS na kuna baadhi ya njia hizi zinafanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android.

Advertisement

Pia hakikisha unasoma makala hii hadi mwisho kwani nitaenda kuonyesha njia ambayo inaweza kusaidia sana kujiokoa mbele za watu hasa unapokuwa unataka kuondoka kwenye eneo ulilopo.

SOS Messages – Android

Kwa kuanza labda tuanze na sehemu ambayo inapatikana kwenye simu nyingi za siku hizi, sehemu hii inaitwa SOS Messages. Inawezekana unaiona sehemu hii kila siku kwenye simu yako lakini hujawahi hata siku moja kujaribu kuitumia, Well kama hujawahi basi sehemu hii ni muhimu sana.

Mara nyingi sehemu hii hupatikana kwenye Settings kwenye ukurasa unaitwa Advanced Features kwa watumiaji wa simu za Android, sehemu hii huruhusu mtu kuweza kutuma ujumbe wa siri kwenda kwa mtu anaye muamini ujumbe ambao utakuwa na data zenye picha, au sauti pamoja na kuonyesha sehemu uliyopo kwa muda huo. Sehemu hii huruhusu kutuma data hizi kimya kimya bila mtu kujua na hutuma data hizo kwa watu pekee ulio wachagua.

Ili kuwasha sehemu hiyo, unatakiwa kuingia kwenye Settings, kisha chagua Advanced Features, kisha angalia mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huo utaona maneno SOS Messages, pia unaweza kutumia sehemu ya kutafuta (Search) iliyopo kwenye ukurasa wa Menu ya simu yako, andika SOS Messages kisha bofya kwenye matokeo na utapelekwa kwenye ukurasa huo moja kwa moja.
Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Pia kama unataka kutumia sehemu hii moja kwa moja ni muhimu kuhakikisha unachagua namba ya mtu ambayo ni ya mtu wako wa karibu kabla ya kutumia sehemu hiyo pale unapokuwa kwenye wakati hatari, ili kuchagua namba unatakiwa kubofya sehemu ya Send Message to, baada ya hapo chagua sehemu unayotaka kati ya Create Contact au Select Contact.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Baada ya kuchagua jina na kuwasha sehemu hiyo sasa utakuwa uko tayari kutumia sehemu hiyo ambayo itakusaidia sana kwenye hali ya hatari, Sasa pale unapokuwa kwenye hali ya Hatari unatakiwa kubofya kitufe cha kuwasha simu yako mara tatu haraka haraka na moja kwa moja meseji yako yenye picha au ujumbe wa sauti au data zenye kuonyesha mahali ulipo zitatumwa moja kwa moja kwa mtu yule ambae ulimchagua awali.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Emergency SOS – iPhone

Kwa upande wa watumiaji wa simu za iPhone pia unaweza kupata sehemu ya kutuma meseji ya kujiokoa kutoka kwenye hali za hatari. Sehemu hii inapatikana kwenye simu zote za iPhone lakini kwa mujibu wa Apple, hatua hizi unaweza kufanya kwenye simu zenye mfumo kuanzia iOS 11.

Sehemu hii inapatikana kwenye App ya Health app ambayo inakuja na simu za iPhone moja kwa moja. Ili kuwasha sehemu hii ingia kwenye App hiyo kisha bofya sehemu ya Medical ID, baada ya hapo bofya Edit kisha angalia kwenye ukurasa huo utaona sehemu imeandikwa Emergency Contacts. Baada ya hapo bofya alama ya jumlisha kuweka namba ya mtu ambae unataka apokee ujumbe pale unapokuwa kwenye tatizo.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Baada ya hapo ili kutuma ujumbe wakati upo kwenye tatizo, bofya kwa kushikilia kitufe cha kuwashia simu pamoja na kitufe cha kupunguza sauti kwa pamoja, utaona imetokea alama ya SOS kwenye kioo chako, bofya kisha slide kidole chako kama unazima simu yoyote ya iPhone.

Jinsi ya Kutumia Smartphone Kujiondoa Kwenye Hali ya Hatari

Kwa kufanya hivyo, mtu uliye kuwa umemuandika kwenye sehemu ya Emergency contact atapokea ujumbe maramoja wenye data kama vile sehemu uliyopo pamoja na data nyingine za muhimu kama tatizo lako ni la kiafya.

Kujiondoa Mwenyewe Kwenye Matatizo

Sasa kama imetokea kwa namna moja ama nyingine unataka kujiondoa mwenye kwenye matatizo au mahali alipo mtu ambaye utaki kuwasiliana nae kwa muda mrefu, ipo App inaitwa Do it Later. App hii inakupa uwezo wa kuseti namba ya mtu yoyote iwe kama inakupigia simu na wewe utajifanya kama umepokea ili kutoka kwenye eneo fulani ambalo hutaki kukaa kwa muda mrefu

Unaweza kuchagua ni muda gani simu hiyo ijipige pia unaweza kuandika jina lolote ambalo unataka litokee juu ya simu yako ikiwa pamoja na namba unayotaka ijitokeze. Unaweza kuseti yote hayo kwa urahisi ndani ya app hiyo, mbali ya hayo app hii inauwezo wa kufanya mambo mengi sana hivyo nakushauri ujaribu kupakua app hiyo alafu tutakuja kuangalia kila sehemu ndani ya app hiyo kwenye makala nyingine. Unaweza kupakua app hiyo hapo chini.

Unknown app
Price: Free

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use