in

Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Nje ya Nchi Kuja Tanzania (Bure)

Kupitia njia hii utaweza kupokea pesa kutoka Nje kuingia kwenye M-Pesa au Tigo Pesa

Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Nje ya Nchi Kuja Tanzania (Bure)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafanya biashara mtandaoni kwa namna moja ama nyingine njia hii inaweza kukusaidia. Pia kama unao ndugu au mtu yoyote anaetaka kukutumia pesa kutoka nje ya nchi na wewe huna akaunti ya benki basi njia hii pia inaweza kukusaidia sana.

Kupitia makala hii nitaenda kukuonyesha kwa ushahidi njia ambayo mimi imeweza kunisaidia kupokea pesa kutoka nje ya nchi bila kupitia benki na pesa yangu kufika kwenye akaunti yangu ya Tigo Pesa (M-Pesa) kwa urahisi na haraka. Bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mambo ya Muhimu

Unacho takiwa kufanya ni kuhakikisha unakuwa na namba ya simu yenye huduma za Tigo Pesa au M-Pesa. Kitu cha muhimu ni kuhakikisha namba yako inafanya kazi kwa asilimia 100 na binafsi ningependekeza zaidi Tigo Pesa kwani ndio huduma ambayo nilitumia na pia ndio ambayo inaonekana kufanya kazi kwa urahisi zaidi.

Hakikisha namba yako imesajiliwa kwa alama za vidole, ili pale tatizo litakapo tokea uweze kufuatilia kwa urahisi na kupata msaada kwa haraka zaidi kutoka kwa wahudumu kwa mteja.

Unatakiwa kumtumia anaye kutumia pesa vitu vifuatavyo,

  • Majina mawili, ila sio lazima jina moja la kwanza ndio muhimu
  • Namba ya simu ambayo unataka kutumia kupokea pesa. Unaweza kuchagua Tigo Pesa au M-Pesa.

Baada ya hapa sasa endelea kwenye hatua hapo chini.

Njia za Kufuata

Kwa kuanza wasiliana na mtu anaetakiwa kukutumia pesa kisha mwambie afuate hatua hizi. Anachotakiwa kufanya ni kubofya Link Hii Hapa, baada ya hapo atapelekwa kwenye tovuti husika kisha mwambie anaweza kufuata maelezo hayo hapo chini. Unaweza kutumia link ya video hiyo.

Kuweza kuelewa zaidi unaweza kuwasha caption ambayo nimeweka kwa Kiswahili, Unaweza kutuma link ya video hii kwa anae kutumia natumaini anaweza kuelewa na kuweza kutuma pesa kwako kwa urahisi na haraka. Mimi nilikua natumiwa dollar $150 na niliweza kuipata kama unavyoweza kuona ujumbe hapo chini ambao nilipokea.

Jinsi ya Kupokea Pesa Kutoka Nje ya Nchi Kuja Tanzania (Bure)

Kama unavyoweza kuona mimi nilifanikiwa kupata pesa kutoka nje ya nchi kuingia kwenye Tigo Pesa kwa urahisi. Kuhusu makato hakuna makato yoyote kwani anae kutumia pesa ndio anayekatwa pesa, lakini pamoja na hayo viwango vya makato ni vidogo sana hivyo nadhani hii ndio njia rahisi na nafuu ya kutuma pesa kutoka nje ya nchi kuja kwenye namba yako ya Tigo Pesa au M-Pesa.

Mbali na njia hii kama wewe unataka kulipwa kupitia njia kama Google Adsense basi unaweza kusoma hapa mahitaji muhimu pamoja na njia za kufuata. Lakini pia kama unataka kutoa pesa kutoka Paypal kuja kwenye akaunti yako ya benki hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kwani kuna njia mpya ambayo tumeanza kufanyia kazi na tutaiweka hapa siku za karibuni.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Simu Yako (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments