in

Mahitaji na Jinsi ya Kupata Mashine ya Risiti ya Kielektroniki (EFD)

Jifunze hapa jinsi ya kupata mashine ya EFD na mambo yanayo hitajika

Mashine ya EFD

Kwa muda sasa nimekuwa nikipata maswali ya jinsi ya kupata mashine ya EFD, ingawa hatua hizi zinapatika kwenye tovuti mbalimbali lakini hebu kwa urahisi kabisa tujaribu kuziandika hapa.

Kwa kifupi kabisa EFD ni mashine zilizotengenezwa kwa ajili ya kutumika katika biashara kwa ajili ya kudhibiti mauzo na mfumo wa mali unaofuata masharti yaliyoelezwa na sheria. Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato mwaka 2012, mtoa huduma hapa Tanzania anapaswa kuwa na mashine ya risiti za kielekroniki (EFD) kuhalalisha mauzo anayofanya.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mashine hizi huunganishwa na mfumo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na kuwasilisha taarifa muhimu ambazo husaidia katika ukadiliaji wa kodi.

Mashine za Risiti za Kielektroniki (EFD) AWAMU YA  PILI

Utekelezaji wa awamu ya pili ya Mashine za  Risiti za Kielektroniki (EFD) ulianza tangu mwaka 2013 kwa lengo la kuongeza idadi ya wafanyabiashara ambao watatumia mfumo wa Mashine za Risiti za Kielektroniki kutoa risiti au ankara za kodi katika kila muamala unaofanyika. Awamu ya pili inajumuisha wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na VAT unasimamiwa chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato, kupitia Kanuni za Kodi ya Mapato (Mashine za Risiti za Kielektroniki), 2012.

Utekelezaji wa awamu ya pili ya Mashine za Risiti za Kielektroniki utajumuisha makundi yafuatayo;

i. Wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa katika kodi ya ongezeko la thamani wenye mauzo-ghafi ya Shilingi milioni 14 na zaidi kwa mwaka;

ii. Wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo maarufu ya Mkoa, waliobainishwa kwa kuzingatia kodi wanayolipa;

iii. Wafanyabiashara wanaoshughulikia sekta za biashara zilizochaguliwa kama vile Vipuli, Vifaa vya Ujenzi, Maduka Madogo, Vituo vya Petroli, Maduka ya Simu za Kiganjani, Maduka madogo ya jumla, Baa na Migahawa, Maduka ya Dawa, Maduka ya Vifaa vya Kielektroniki, nk.

Mfumo huu utaendelea na Mamlaka itakuwa inasajili taratibu wafanyabiashara kulingana na ustawi, uzoefu na uwezo wa biashara za wafanyabiashara hao

Kupata mashine za risiti za kielektroniki ni rahisi sana unahitaji kuwa na mambo machache sana ili uweze kuwezesha kupata mashine hiyo.

Kifupi Mahitaji ya EFD ni Haya

Kwa kampuni Unahitaji vyote hivyo hapo juu pamoja na 

Na hayo ndio maelezo mafupi jinsi ya kupata mashine hiyo ya EFD au Electronic Fiscal Devices, kama unataka maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti ya TRA au piga simu za bure kwa Tanzania 0800 750 075 au 0800 780 078.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Mahitaji na Jinsi ya Kupata Mashine ya Risiti ya Kielektroniki (EFD)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.