Jinsi ya Kupunguza Matumizi Internet Kwenye Simu Yako

Je simu yako inamaliza (data) kwa haraka bila we kujua.? basi soma hii
data internet data internet

Internet ni kitu cha msingi kwenye smartphone yoyote ila pale inapotokea unamaliza kifurushi chako cha data bila kujua kiukweli unakua huna hamu tena na kampuni uliyonunulia (data) au bando, hii inatokea kwa kuhisi labda ni mitandao hiyo ndio yenye kukupa kifurushi ambacho akija kamilika, lakini hii si kweli.

Simu nyingi za sasa zinauwezo mkubwa wa kuwasha programu mbalimbali ambazo hizi ndio hutumia (data) internet ya simu yako bila wewe kujua pia programu nyingine hutumia kiasi kikubwa cha data hata kuliko tunavyodhani. Kwa mfano programu ya Instagram: instagram imeonekana kutumia asilimia 30% mpaka 50% ya kifurushi chako cha data vilevile kuna zingine kama Youtube na Google Services (hii ni programu inayosaidiana na google play store, inakuwa sambamba na Play Store pale unaponunua simu yako) baadhi ya hizi programu ni muhimu kwa matumizi ya kila siku na zingine ni muhimu ili simu yako ifanye kazi inavyotakiwa, hapo ndipo tunapojiuliza je tutafanyaje..?

Advertisement

leo tunaenda kujifunza namna ya kupunguza matumizi ya (data) internet kwenye simu yako kwa urahisi kabisa, unachohitaji kufanya ni  kuwa na kifurushi cha data kiasi cha  MB100 na kuendela pia ni lazima uwe unatumia simu yenye kutumia systeam ya undeshaji ya Android, kisha fuata hatua hizi.

Hatua ya kwanza pakua programu ya Opera Max kwa kubofya hapo chini kisha fuata hatua zote hapo juu kwenye video iliyoko hapo juu.

Jinsi ya kutumia programu hii ni rahisi kabisa na nimuhimu sana kuwa na programu hii kwenye simu yako ya Android kama utashindwa kutumia progamu hii usisite kutuandikia kwenye maoni au kwenye mitandao yetu ya kijamii.

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use