Jinsi ya Kubadilisha Instagram Kuwa ya Kibiashara

Jifunze Namna ya Kubadili Akaunti yako ya Kawaida ya Instagram kuwa ya kibiashara
instagram-ya-kibiashara instagram-ya-kibiashara

Hivi karibuni Instagram ilitangaza kuleta akaunti za kibiashara kwenye mtandao huo bora wa kijamii, hata hivyo hivi karibuni kumeonekana baadhi ya watu waliofanya update kwenye programu hiyo wamepata uwezo wa kubadilisha akaunti zao za kawaida kuwa akaunti za kibiashara.

Leo tanzania tech tunakuletea namna rahisi ya kubadilisha akaunti ya kawaida ya instagram kuwa akaunti kamili ya kibiashara yenye muonekano wa tofauti kabisa na akaunti ya kawaida, basi kwa kuanza ili kubadilisha akaunti yako ya instagramu kuwa ya kibiashara unaitaji baadhi ya mambo yafuatayo.

Jambo la kwanza hakikisha akaunti ya Instagram unayotaka kubadilisha kuwa ya kibiashara inayo profile kwenye mtandao wa facebook kwani Instagram inatumia akaunti ya facebook kukamilisha usajili wa akaunti yako ya kibiashara kwenye mtandao wa Instagram, baada ya hapo hakikisha pia programu yako ya Instagram inaenda na wakati yani iko (updated) baada ya hapo fuata maelekezo haya.

Advertisement

Hakikisha unafuata maelekezo haya kwenye video hiyo hapo chini baada ya hapo utakua na uwezo wa kuona akaunti yako ya kibiashara ya instagram.

Kama unataka kujifunza zaidi endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use