Simu Mpya ya Tecno Camon X Kuzinduliwa Rasmi April 5

Jiandae na kamera mpya ya kisasa kupitia simu ya Camon X
Camon X Camon X

Baada ya tetesi za ujio wa simu mpya za Tecno Camon X pamoja na Camon X Pro sasa habari tulizozipata hapo jana zinadhibitisha kuwa, simu hizo mpya zitazinduliwa rasmi tarehe 5 Aprili mwaka huu 2018 na uzinduzi rasmi unategemewa kufanyika huko nchini Nigeria.

Advertisement

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, simu hizo zinategemewa kuja na kamera zenye nguvu zaidi na zinategemewa kuja na sifa za tofauti kuliko simu zingine za Tecno Camon. Mbali na hayo Bado hakuna taarifa zaidi za sifa kamili za simu hiyo lakini tutaendelea kuwaletea habari kamili za simu hii, ikiwa na uzinduzi wa simu hii mubashara kabisa.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *