Samsung Electronics imezindua rasmi Galaxy S26 series nchini Tanzania, ikiongozwa na Galaxy S26 Ultra ambayo inaleta ubunifu wa kipekee katika sekta ya simu za mkononi kupitia teknolojia mpya ya Privacy Display iliyomo ndani yake. Hii ni mara ya kwanza kwa simu ya mkononi kuwa na mfumo wa kulinda faragha moja kwa moja kwenye skrini yake, ikiimarisha usalama wa taarifa binafsi katika mazingira ya kila siku.
Katika dunia ya leo ambapo simu inabeba taarifa nyeti kama miamala ya kifedha, nywila, mazungumzo binafsi na taarifa za kazi, Galaxy S26 Ultra imeundwa kulinda kila kitu kinachoonekana kwenye skrini yako. Teknolojia ya Privacy Display inazuia watu waliokando yako kuona kwa urahisi kile unachofanya, iwe uko kwenye usafiri wa umma, mgahawani au kwenye mkutano.

Mtumiaji anaweza kuchagua ni wakati gani kipengele hiki kiwashwe, hasa anapoingiza nywila, kufungua programu maalum au kushughulikia taarifa za siri. Hii si tu ulinzi wa kawaida wa programu, bali ni ulinzi unaoanzia kwenye pikseli za skrini yenyewe.
Mbali na ulinzi wa kimwili wa skrini, Galaxy S26 Ultra pia imeimarishwa kwa tahadhari za faragha zinazoendeshwa na akili mnemba. Simu inaweza kumuarifu mtumiaji pale programu zinapojaribu kufikia taarifa nyeti kama eneo halisi au mawasiliano bila sababu ya msingi, hivyo kumpa udhibiti na uwazi zaidi juu ya matumizi ya taarifa zake.
Pamoja na kuimarisha faragha, Galaxy S26 Ultra inaendeleza ubora wake katika upigaji picha, hasa katika mazingira ya mwanga hafifu. Lenzi zilizoimarishwa na uwezo wa kupokea mwanga zaidi hutoa picha nzuri zaidi hata wakati wa usiku au ndani ya majengo yenye mwanga mdogo. Teknolojia ya Nightography Video inahakikisha video zinabaki na rangi halisi na mwonekano safi hata baada ya jua kuzama, iwe ni katika hafla za usiku, matamasha au mikusanyiko ya familia. Uboreshaji wa Super Steady nao unaongeza uthabiti wa video hata unapokuwa kwenye mwendo.

Galaxy S26 Ultra pia imejengwa juu ya msingi wa akili mnemba ya hali ya juu inayofanya kazi na kurahisisha maisha ya mtumiaji. Simu inaweza kupendekeza picha husika pale zinapohitajika, kukagua ratiba za mikutano pindi ujumbe unapozitaja, au kukumbusha vitu vya muhimu kulingana na matumizi ya kila siku. Kwa kuunganishwa na huduma za AI kama Gemini na Perplexity, Galaxy S26 Ultra inamwezesha mtumiaji kukamilisha majukumu kwa urahisi kupitia sauti au kitufe kimoja tu.
Kifaa hiki kinaendeshwa na kichakataji chenye nguvu cha Snapdragon 8 Elite Gen 5 Mobile Platform for Galaxy, kinachohakikisha matumizi yanakuwa ya kasi, rahisi na ya kuaminika siku nzima. Pia kina teknolojia ya kuchaji kwa haraka nakuweza kufikisha betri hadi asilimia 75 ndani ya dakika 30, hivyo kupunguza muda wa kusubiri.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Biashara za Simu wa Samsung Tanzania Mgopelinyi Kiwanga, alisema Galaxy S26 Ultra imetengenezwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya watumiaji wa leo. “Katika kipindi ambacho simu imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku, faragha si chaguo tena bali ni hitaji. Kupitia Privacy Display na maboresho ya akili mnemba (AI), Galaxy S26 Ultra inampa mtumiaji uhakika kwamba taarifa zake zinalindwa wakati wote,” alisema.
Galaxy S26 Ultra, S26+ na S26 zinapatikana kwa oda ya mapema katika maduka yaliyoidhinishwa ya Samsung na washirika wake nchini kote. Simu hizi zinapatikana katika rangi za Cobalt Violet, White, Black na Sky Blue.
Bei elekezi ya Galaxy S26 Ultra 512GB ni TZS 4,305,000 huku toleo la 256GB likiuzwa kwa TZS 3,672,000. Galaxy S26+ 512GB inauzwa kwa TZS 3,864,000 na 256GB kwa TZS 3,190,000. Galaxy S26 ya kawaida inapatikana kwa TZS 2,627,000.
Kwa kulinda zaidi thamani na ubora wa kifaa chako, Samsung Care+ inalinda uwekezaji wako kupitia kinga dhidi ya uharibifu wa bahati mbaya kama kuvunjika kwa skrini, dhamana ya miezi 24 na huduma ya wataalamu waliobobea katika vituo vilivyoidhinishwa nchini kote, ikikupa uhakika kwamba uko salama hata pale mambo yasiyotarajiwa yanapotokea.

