Hizi Hapa Picha Zaidi za Nokia X au Nokia X6 (2018) 1

Hizi Hapa Picha Zaidi za Nokia X au Nokia X6 (2018)

Kama tulivyo sema wiki hii, Nokia inategemea kurudi tena na simu yake ya Nokia X au Nokia X6 (2018) ambayo inasemekana kuja na muonekano wa kisasa huku ikiwa na ukingo wa juu maarufu kama Notch.

Sasa muda mchache kabla ya kutoka rasmi kwa simu hiyo ya Nokia X tumefanikiwa kupata picha za simu hiyo ambazo zimesambazwa kupitia mtandao wa Weibo wa nchini china. Hizo hapo chini picha zaidi za simu hiyo inayo tarajiwa kuzinduliwa leo siku ya ijumaa nchini China.

Kama inavyo onekana kwenye picha ya mwisho hapo chini, simu hiyo imepewa model namba ya TA-1099 na vyanzo vingine vya habari vinasemekana simu hiyo inategemewa kutambulishwa rasmi kwa nchi nyingine kuanzia tarehe 16 mwezi ujao (May). Kwa sasa bado hakuna taarifa kamili kama simu hiyo imesha zinduliwa rasmi, endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea taarifa kamili pindi tu tutakapo zipata.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Oppo A3 (2018)
Zifahamu Hizi Hapa Sifa za Simu Mpya ya Oppo A3
Next Post
App za kupima uwezo wa simu

Apps# 9 Hizi Hapa App Nzuri za Kupima Uwezo wa Simu Yoyote